KIPINDI CHA MACHOZI KATIKA NDOA


NDOA INA VIPINDI VIKUU VINNE;

1; Penzi Penzini ( love Season)
2; Machozi na Vilio;( Crying Season)
3:Amani na Utulivu ( Peace Season)
4; Uzeeni - Miaka 50 ya ndoa na kuendelea;

Wiki iliopita Nilianza na Crying Season, Kipindi cha Machozi Zile comment 2000 Zimenionesha kitu, Mimi na mke Wangu Celestina Tumekujadili Tumekuombea;

Naomba Uniruhusu leo, Niendelee na Kipindi hiki cha Machozi. Najua upo hapa, Umekataa tamaa, Umetumani kuondoka, mwingine kihisia, Kimwili Umeondoka  huwa ni kipindi cha Muda tu kama Ukieleweshwa;

TABIA ZA KIPINDI HIKI;
1; Uzuri wa nje ulie kuvutia siku za Mwanzo. Urefu, Shape, Rangi, Miguu, Kifua, Mkono, Macho, Huwa havionekani tena
Unaona Mtu kenge, Fisi, Mbaya, Ndo ile kauli ilizaliwa hapa
Wanaume wote Mbwa, Wanawake wote Pasua kichwa, Vivuruge PRO +….

2;Kipindi hiki zile lugha, Najuta kuwa na wewe, Sikujua uko hivi, Umebadilika sana, Najutaaaa ! I wish I would know you such a bad person; 

3;Hakuna kuogopana, Hakuna kufichiana siri, Mwanandoa anaweza kuropoka udhaifu wa mwenzie Hadharani 
Kama hamna utaratibu wa Ku shughulikia mambo yenu, Mnaweza tupiana maneno mbele ya watoto,watu mnaoishi nao. Ndugu hata mbele ya halaiki

4;Hakuna Mawasiliano siku nzima mnakutana Home Usiku tu
Mtu akipita kwenye 18 za Mtu anaweza chezea kichambo hatari, hata Makofi 

5;Hakuna kujaliana upo wapi, Upo na nani
Wanandoa huanza kuchepuka hapa, na wale waaowaona wa na wajali; 

6;Kwa mwanaume, kipindi hiki ni cha Mapambano kweli kweli, kutengeneza Dira ya Familia, Kutafuta School fees, kutamani kuwa na kiwanja, Gari.. wanaume huwa wanaanza kutafuta njia zisizo halali ili Dira ya familia ipatikane 
Hakuna ufundi wa tendo la ndoa,  hakuna hisia!
Yaani vurugu; Mwanaume akirudi home mke hamwelewi; Mwanaume Analia ndani kwa ndani, wengi wanachelewa kurudi kuepusha virugu,  wengine wanaanza ulevi, michepuko sababu atatafuta pakupumulia;

7;Mwanamke anapambana na ulezi, watoto ndio kipaumbele haitaki Tendo la ndoa anaona Miyeyusho tu; Kipaumbele watoto tu, hamwoni Mwanaume, kujaliwa hakuna, anadhami upendo umeisha, Vurugu mtindo mmoja;

Rafiki yangu Mpendwa hiki ni kipindi cha muda tu, KINAISHAGA; VUMILIA; Ongeza Maombi

Usiondoke kwa huyo; Bado Anakupenda
Ni Kipindi cha Pili cha kwenye Ndoa

Usiache Mbachao kwa  Msala Upitao 
Vinaishaga hivi; kaza Buti, Songa Mbele Ndugu yangu;



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

Wasifu wa Kizza Besigye

NAMNA YA KUTENGENEZA MAISHA YAKO KIMYA KIMYA

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA

HAKUNA DHEHEBU LA DINI AMBALO LIKO JUU YA LINGINE, MADHEHEBU YOTE YAKO SAWA KISHERIA - RAIS SAMIA