SERIKALI KUPELEKA UMEME MITAA 14 ILIYOSALIA TARIME MJINI


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imepanga kupeleka umeme katika mitaa 14 iliyosalia bila huduma hiyo katika Mji wa Tarime, kwa kuhakikisha mitaa yote inafikiwa na umeme.


Salome amesema hayo leo, Juni 8, 2026, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, aliyetaka kujua ni lini umeme utafika katika mitaa yote isiyo na umeme katika Mji wa Tarime.


Amesema Mji wa Tarime una jumla ya mitaa 81, ambapo mitaa 54 ina umeme na mitaa 27 haina umeme.


Amefafanua kuwa kati ya mitaa 27 isiyo na umeme, mkandarasi anaendelea na kazi katika mitaa 13 na hadi sasa ameshasimamisha nguzo huku akijiandaa kuanza kufunga nyaya.


Aidha, Salome amesema Serikali kupitia TANESCO imepanga kupeleka umeme katika mitaa iliyosalia kulingana na upatikanaji wa fedha, kwa lengo la kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kila mtaa nchini umefikiwa na huduma ya umeme.


Kadhalika, Salome ametumia nafasi hiyo kueleza mipango ya Serikali ya kumaliza changamoto ya kukatika kwa umeme katika Mji wa Tarime na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika migodi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA