NA: MWANDISHI WETU, PANGANI Viongozi na watendaji wa matawi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Pangani mkoani Tanga, wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa masuala mbalimbali ya kichama, kiuongozi na kijamii ili kuboresha utendajikazi wao wa kila siku. Mafunzo hayo yametolewa Agosti 2, 2026, katika Kata ya Kipumbwi wilayani humo. Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Seneti ya vyuo vya kati, vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Tanga, Leila Mnaki, ambaye alikuwa miongozo mwa wakufunzi, amesema CCM ni Chama imara kwani misingi yake ipo ngazi za chini za mabalozi na matawi, hivyo ni wajibu wa Chama kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa viongozi wake ili kuboresha utendajikazi. "Nguvu ya Chama ni wanachama na viongozi wake, ndiyo maana tupo hapa kupata mafunzo ya kutujengea uwezo ili utendajikazi wetu uwe wenye tija kwa manufaa ya Chama na wananchi tunaowahudumia," amesema Mnaki. Aidha, Mnaki amesema, ni wajibu wa viongozi kuwahudumia wananchi kwa kufuat...
Comments