Mabanda ya Benki ya NMB yanaendelea kuwa miongoni mwa vivutio vikuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika kanda mbalimbali nchini, huku mawaziri, viongozi wa Serikali na Wananchi wakitembelea kujionea suluhisho za kifedha zinazowezesha kilimo, mifugo, uvuvi na biashara.
Waziri
wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, na Naibu Waziri wa Kilimo, David
Silinde, wakitembelea banda la Benki ya NMB wakati wa Maonesho ya Nane
Nane yanayoendelea jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, akimsikiliza Meneja Mahusiano wa
Benki ya NMB Kanda ya Kati kutoka Idara ya Kilimo na Biashara, Miastela
Magoma, alipokuwa akipata maelezo kuhusu huduma za benki hiyo
alipotembelea banda la NMB kwenye Maonesho ya Nane Nane Kanda ya
Mashariki yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere,
mkoani Morogoro.

Mwanza:
Meneja Mahusiano wa Biashara kwa Serikali wa Benki ya NMB, Humphrey
Kaaya (kushoto), akitoa maelezo kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuhusu
fursa za upatikanaji wa mikopo ya matrekta na suluhisho za kifedha
zinazowezesha ununuzi wa zana za kisasa za kilimo, wakati wa Maonesho ya
Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo, mkoani Mwanza.
NMB
ni mdhamini wa Maonesho ya Nane Nane 2026, ikiwa sehemu ya dhamira yake
ya kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi na kuwawezesha
wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali kuongeza tija na kukuza
uchumi kupitia huduma zinazokidhi mahitaji yao.






Comments