TAMISEMI YASOGEZA UTOAJI WA HUDUMA YA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE DODOMA

 


NA OWM - TAMISEMI, DODOMA

OFISI ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali - TAMISEMI imeendelea kusogeza   utoaji wa  huduma ya elimu kwa wananchi.


Mkurugenzi Msaidizi wa Sekta za Uchumi na Uzalishaji  Tawala za Mikoa Ofisi ya Waziri  Mkuu- TAMISEMI Mhandisi Enock Nyanda amesema TAMISEMI inaendelea  kusogeza huduma kwa wananchi sababu ni Wizara ambayo moja kwa moja huduma zake zinaenda kwa wananchi ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu, Kilimo na Miundombinu.


Amesema hayo jana Agosti 03, 2026 katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea viwanja vya John Malecela  Jijini Dodoma.


"  Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI ni miongoni mwa

Wizara za Mwanzo zilizoanzishwa mara baada ya kupata Uhuru mwaka1961 hivyo mengi mazuri yamefanyika katika kipindi chote, " ameeleza Mhandisi Nyanda.


Mhandisi Nyanda amebainisha hayo baada ya  mwanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi  Gloria, iliyopo Ihumwa Jijini Dodoma,kuuliza Wizara ilianzishwa lini  walipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu  TAMISEMI.


Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea  maonesho ya nanenane katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI pamoja na taasisi zake ikiwemo TARURA, DART, Shirika la Masoko  Kariakoo, Tume ya Utumiwa wa Walimu, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAAFISA JENERALI WASTAAFU 17 WA JWTZ WAAGWA.

JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA

BINTI WA KITANZANIA GLORIA MAJULE ASHINDA TUZO YA UANDISHI BORA WA FILAMU YA MALARIA MAREKANI ‎

HII NDIYO CV YA KOCHA MPYA WA YANGA

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

CDF MKUNDA AWATAKA MAAFISA JENERALI WASTAAFU KUACHA KUHANGAIKA NA SIASA

PICHA YA RAIS ILIYOBAMBA WIKI HII