Mmoja wa majeruhi akiwahishwa kupata tiba hospitali baada ya Gari la Abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 373 BGT linalofanya safari zake katika barabara ya Moshi-Arusha, ambalo limesababisha ajali kwa kugongana na basi la Ngorika linalofanya safari za Arusha- Dar. Watu kumi walifariki katika ajali hiyo. (PICHA NA AMRI MVUNGI).
WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wasiosomea masuala ya Kilimo kuuza pembejeo. Amesema kuwa masharti ya muuza pembejeo lazima awe amesomea Kilimo kwa ngazi ya cheti, diploma na Digrii. Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wadau wa mbegu katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma. "Haiwezekani wanaowashauri na kuwauzia mbegu wakulima wasiwe na utalaamu wa sekta hiyo, mbona wanaogawa dawa na kutibu wagonjwa wamesomea ufamasia, uuguzi na udaktari, kwa nini isiwe kwenye Kilimo? Amehoji Waziri Bashe. Amewapa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja wauzaji kwenda kusomea Kilimo ili waruhusiwe kisheria kuuza Pembejeo na kwamba baada ya hapo sheria itafuata mkondo wake kwa kukagua maduka yote ya pembejeo na kuwakamata watakaobainika.
Comments