ASKARI JESHI KIKOSI CHA ANGA WATEMBELEA TBL

 Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Anga, akiingia kutembelea kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea jinsi bia zinavyozalishwa pamoja na kujifunza masuala ya Usalama mahali pa kazi, afya ya wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Kitengo cha Sheria wa TBL, Steve Kilindo, akitoa maelezo kwa maaskari hao kuhusu historia ya kampuni hiyo.
 Meneja wa Masuala ya Usalama mahali pa kazi wa TBL, Renatus Nyanda, akielezea kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji wa bia kiwandani hapo.
 Steve Kilindo akisalimiana na maofisa wa kikosi hicho cha Anga
 Askari wakitembelea kiwanda hicho kilichopo Ilala. Mchikichini, Dar
                                               Wakiangalia unga wa mahindi unaotumika kutengenezea bia
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, wakimsikiliza Mtaalamu wa Upishi wa bia, Richard Kagosi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emanuel Festo (kushoto), akiwaeleza jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia kompyuta   walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.
Meneja Ubora wa Bidhaa za TBL, Lydia Soi akitoa maelezo jinsi wanavyodhibiti ubora wa bidhaa kiwandani hapo
Mtaalamu wa upishi wa bia wa TBL, Emmanuel Sawe akiwapa maiwa katika matangi hayo.elezo askari jinsi bia inavyochachuliwa katika eneo hilo la matangi.
Askari wakitembezwa eneo la matangi yanayotumika kuchachulia bia
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Your Solutions Tanzania Limited, George Damian akionesha kifaa cha kisasa cha kuzimia majanga ya mato yanapotokea/
Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, akielekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni yaYour Solution Tanzania Limited, Damian George, jinsi ya kukitumia kifaa cha kisasa cha kuzimia moto kiitwacho DSPA, walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Anga, wakiangalia kifaa cha kisasa cha kuzimia moto  kiitwacho DSPA cha kampuni ya Your Solution Tanzania Limited, walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujifunza masuala ya usalama kazini, afya kwa wafanyakazi na utunzaji mazingira.

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kitengo cha Anga, akielekezwa na Mtaalamu wa masuala ya usalama kazini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, jinsi ya kukitumia kifaa cha kisasa cha kuzimia moto kiitwacho DSPA, walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira. Kifaa hicho kinaingizwa nchini na Kampuni ya Your Solution Tanzania Limited.
Askari wakisikiliza kwa makini walipokuwa wakipata maelezo ya jinsi ya kukitumia kifaa hicho cha kuzimia moto

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS