Diamond
Vs Ali Kiba ni ushindani usio rasmi unaochochewa zaidi na mashabiki wa
muziki Tanzania kwa kuwa wawili hao licha ya kuwa wote ni wasanii wenye
uwezo mkubwa sana kwenye uimbaji wanatajwa kuwa na tofauti au vita
baridi.
Wapo wengi ambao wanauzungumzia hata kama sio kwenye vyombo vya habari
na kuna wachache ambao maoni yao yamefika kwenye vyombo vya
habari.Vijimambo imezungumza na mmiliki wa G Records, Guru Ramadhani aka
DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha
kwenye mkondo mkubwa wa muziki ametoa maoni yake kuhusu utofauti
anaouona kati ya wasanii hao.
“Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata
katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba
vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana
sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi.” Amesema
G-Lover.Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally Kiba yuko juu kupitia studio
yake alikuwa na team ya watu wasiopungua thelathini, kitu ambacho
Diamond anakifanya sasa hivi.Lakini unapokuja kibiashara Diamond huwa
anazungumza kuwa yeye muziki wake anaufanya kibiashara na ndo maana ana
team work kubwa ambayo inamsaidia yeye kujua ni kitu gani anatakiwa
kufanya, kuna kitu gani anatakiwa kukifanya kwa upande wa muziki. Sasa
kwa upande wa Ali kwa sasa hivi, kwa kipindi niko naye nilikuwa na team
ambayo hata yeye alikuwa hajui mimi nipo na akina nani nyuma yangu.
Alikuwa anajua kuwa yupo G, lakini nyuma yangu nilikuwa na watu takriban
thelathini ambao ni team work ambayo ilikuwa inafanya kazi kwa Ali Kiba
kujua ni kitu gani na kitu gani tunatakiwa tufanye ili afike na mpaka
akafika hapo. Ameeleza.
“Diamond
naye anafanya vitu kama hivyo, unaweza kuona Diamond ana team ya watu
watatu tu au wanne ambao wanamsaidia, kwahiyo utaona Diamond kuna watu
kibao ambao amewapa ajira. Kwahiyo Diamond hawezi kuwaangusha watu ambao
wapo nyuma yake ambao wamepata ajira kutoka kwake. Kwa mfano kuna
utofauti mkubwa ambao Diamond amekuja nao ambao ukiangalia ni utaratibu
uleule ambao nilikuwa nikiufanya kwa Ali. Kwahiyo sijui kuna utofauti
gani kati ya management ya Diamond na ya Ally Kiba ya sasa hivi.
Comments