KAMBI YA MAFUNZO ELEKEZI KWA VIONGOZI 120 WA TGGA YAZINDULIWA KILIMANJARO+video

 

Girl Guides wakiimba na kucheza wakati wa ufunguzi wa Kambi ya mafunzo elekezi kwa viongozi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) katika Shule ya Sekondari ya  Ufundi  Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo yanashirikisha viongozi kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani.
Washiriki wakipata maelezo jinsi ya kuitengeneza pamoja na kuitumia Bendera ya TGGA.Mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa siku 6.
Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Maembe  akizungumza  alipokuwa akifungua kambi ya mafunzo kwa viongozi wa TGGA, Kulia kwake ni Kamishna Mkuu wa TGGA,Symphorosa Hangi na Mwenzekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro.TGGA imetimiz.a miaka 93 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo, Anna Maembe (kulia) Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (katikati) na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kamishna Mkuu wa TGGA,Symphorosa Hangi  akiwasalimia viongozi  na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo ya mafunzo..
Washiriki wakipiga makofi baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgeni rasmi, Anna Maembe.

Washiriki wakiwa katika mafunzo kwa vikundi
Mratibu wa Programu za TGGA, Valentina Gonza akiongoza mafunzo wakati wa kambi hiyo.
Baadhi ya viongozi  wakitambulishwa
Mwenyekiti wa Vijana wa TGGA, Tanga, Valentina Mohindo akisoma risala kuhusu mafunzo hayo.
Mmoja wa viongozi wa TGGA  kutoka Zanzibar akiburudisha washiriki kwa kuimba utenzi.


Skauti wakipita kujitambulisha.
Kamishna wa Skauti Wilaya ya Moshi, Emernsiana Mbeno akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi Anna Maembe akizawadiwa kikombe cha kumbukumbu
Mgeni rasmi akizawadiwa saa
Mgeni rasmi akiwa katika picha za pamoja na viongozi mbalimbali wa TGGA na wageni waalikwa








Kamishna wa TGGA Bagamoyo, ambaye pia ni mshereheshaji wa Kambi hiyo, MC Mamyto, Martha Mshiu (Kushoto)  akiwa na Kamishna Mkuu,Symphorosa  Hangi (kulia) pamoja na mgeni rasmi, Anna Maembe.


 Kamishna msaidiyi Mkuu wa TGGA, Sara Milunga (katikati) akiwa na Kamishna Mkuu, Symphorosa  (kulia) pamoja na mgeni rasmi, Anna Maembe.PICHA YOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video Mgeni rasmi Anna Maembe akihutubia baada ya kusikiliza risara ya viongozi wa TGGA wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo.....

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU