SIMBACHAWENE: POLISI WAACHENI WATUHUMIWA WATUMIE SIMU KUWAJULISHA NDUGU ZAO+video


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene leo Novemba 26, 2021 amezungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu tulipotoka, tulipo na tunakoelekea na kuelezea changamoto na mafanikio kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofikia kilele Desemba 9,2021.


Simbachawene ameelezea mambo mbalimbali kuhusu mafanikio ya wizara hiyo, lakini pia amewatahadharisha polisi wasio waaminifu wanaowanyima watuhumiwa kutumia simu zao au za kituo cha polisi kuwajulisha ndugu zao kwamba wamekamatwa, amewataka kuacha mara moja tabia hiyo na atakayekiuka atachukuliwa hatua kali... 


Ofisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Immaculate Makilika akiwa na baadhi ya maafisa wa wizara ya Mambo ya Ndani wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Simbachawene  akizungumza na wanahabari. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kusikiliza wakati Waziri Simbachawene akielezea mafanikio ya wizara hiyo.




Mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha ITV Dodoma, Shaban Tolle akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.
Mwandishi wa habari wa Macho Media Online TV, Ahmad Said  akiuliza swali kwa Waziri Simbachawene.

Ofisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Immaculate Makilika (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Simbachawene baada ya mkutano huo aliouongoza kumalizika. 


Mwandishi wa habari wa Macho Media Online TV, Ahmad Said akiuliza swali kwa waziri wakati wa mkutano huo.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Simbachawene pamoja na mambo mengine akipiga marufuku polisi kuwanyima watuhumiwa kuwasiliana na ndugu zao kwa simu wawapo vituo vya polisi..



 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.