BALOZI WA CHINA KUPITIA DKT. MAJULE APELEKA NEEMA KWA WANAWAKE DODOMA

 Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian amekabidhi msaada wa cherehani 120 kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa huo, Dkt. Neema Majule kwa ajili ya kuzigawa kwa wanawake wa Dodoma Mei 27, 2026.

Balozi Mingjian na Dkt. Majule wametiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya wanawake wa China na wanawake wa Mkoa wa Dodoma katika hafla iliyofanyika Ofisi za Mbunge huyo zilizopo Shule ya Rhema mkoani humo. Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Mingjian amesema China itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania hususan katika kuwawezesha wanawake na kuongeza fursa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Ameeleza kuwa uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China umeendelea kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuinua maisha ya wanawake.

Kwa upande wake, Dkt. Majule ameishukuru Serikali ya China kwa msaada huo akisema cherehani hizo zitasaidia wanawake wengi wa Dodoma kujiajiri, kuongeza kipato na kuboresha maisha ya familia zao.

Amesema ushirikiano huo ni hatua muhimu ya kuwainua wanawake kiuchumi na kuwapa nafasi zaidi ya kushiriki katika shughuli za maendeleo

Balozi Mingjian na Dkt. Majule wametiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya wanawake wa China na wanawake wa Mkoa wa Dodoma
Balozi wa China akikabidhi msaada huo kwa Dkt Majule.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA