MBUNGE MTATURU AHIMIZA UMOJA NA MSHIKAMANO, ACHANGIA CHEREHANI 10.


 


  


Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki Sherehe za Maadhimisho ya Mwaka Mmoja tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kiislamu( Almadrasatul Tah Dhiibul Islaamiyaa na kuwahimiza viongozi wa dini kuhubiri Umoja na mshikamano.

Aidha,amechangia Cherehani 10 na Seti moja ya Kujifunzia Ufundi Seremala kwa vijana wa chuo hicho.

Akizungumza Disemba 4,katika maadhisho ya chuo hicho kilichopo Kata ya Dung’unyi Wilayani Ikungi,Mtaturu amesema Umoja na mshikamano ukiwepo utachagiza maendeleo.

“Nimefurahishwa na mafunzo mnayofundishwa Vijana hapa, nami kama muwakilishi wenu nawaunga mkono kwa kuwachangia Cherehani 10 na Seti moja ya kujifunzia ufundi Seremala,

Amewaomba wananchi kuliombea Taifa ili kupata mvua na kuondokana na tishio la Ukame.

Mhe Mtaturu ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kata ya Dung’unyi kupata Milioni 80 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa katika Shule za Sekondari Dadu na Munkinya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA

JESHI LA POLISI LATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA, LAONDOA KIZUIZI CHA KUTOTOKA NJE BAADA YA SAA 12 JIONI