SHULE YA PAMOJA YA ARUMERU WAFUNDISHWA BUNGENI UHUSIANO WA BUNGE NA RAIS, UMUHIMU WA SIWA+video


Mtumishi wa Bunge, Waziri Kizingiti akitoa mafunzo kwa wananfunzi kuhusu uhusiano wa Bunge na Rais na umuhimu wa rungu au Siwa bungeni.

Afisa Habari wa Bunge, Zanele Chizza akiongoza mafunzo hayo.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Dkt. John Pallangyo akiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii, nidhamu ya hali ya juu na kuwa na hofu ya Mungu ili wafanikiwe katika maisha yao.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Pamoja iliyopo Arumeru Arusha, wamefarijika na mafunzo waliyopata wakati wa ziara yao bungeni Dodoma Juni 9,2022.

Wanafunzi hao wameonesha furaha yao walipozungumza wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na Mtumishi wa Bunge, Waziri Kizingiti kwa kushirikiana na Afisa Habari wa Bunge, Zanele Chizza katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Dkt. John Pallangyo ambaye ni miongoni mwa waliofanikisha ziara hiyo, amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii pamoja na kuwa na hofu ya Mungu ili wapate mafanikio makubwa katika maisha yao.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Wanafunzi wakipata mafunzo hayo...


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO TV/BLOG
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NG'OMBE 'KIKWETE' AWA KIVUTIO MAONESHO YA NANE NANE DODOMA

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

DUWASA IMEJIPANGA VILIVYO KUHUDUMIA WANANCHI MAONESHO YA NANE NANE NZUGUNI DODOMA+video

GLOBAL DISCUSSION TOPIC ON: GLOBAL GREEN ECONOMIIE VS GLOBAL ENERGY SHORTAGE

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

RC MTAKA: KARIBUNI NJOMBE MWANDAE PENSHENI ZENU KWA KUPANDA MITI, PARACHICHI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

REKODI YA SIMBA NA YANGA TANGU MWAKA 2010

RC SENYAMULE ATAMANII DODOMA IWE NA MUONEKANO WA KIMATAIFA+video

MAKAMU WA RAIS, DKT MPANGO AZINDUA MITAMBO YA KISASA YA UCHORONGAJI YA STAMICO