NECTA YATANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) ULIOFANYIKA MEI, 2022

                                                         

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Jumanne, Julai 5, 2022, limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) huku likisema kulingana na matokeo hayo ufaulu umepanda ikilinganishwa na mwaka jana.


NECTA imetangaza matokeo hayo katika Mkutano wake wa 147 uliofanyika leo Julai 5, 2022 katika ukumbi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA) mjini Zanzibar, ambao uliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika tarehe 09 - 27 Mei, 2022.

Taarifa iliyotolewa na NECTA imesema, Jumla ya watahiniwa 95,826 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha
Sita Mei, 2022 wakiwemo wasichana 41,517 (43.33%) na wavulana 54,309 (56.67%) na kwamba kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa Shule walikuwa 85,414 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 10,412.

Imesema taarifa hiyo kwamba, kati ya watahiniwa 95,826 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha
Sita Mei, 2022, watahiniwa 94,456 sawa na asilimia 98.57 walifanya mtihani na watahiniwa 1,370 sawa na asilimia 1.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za Ugonjwa na Utoro.

Kwa Watahiniwa wa Shule, kati ya watahiniwa 85,414 waliosajiliwa, watahiniwa 84,870 sawa na asilimia 99.36 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 37,468 (99.54%) na wavulana 47,402 (99.23%). Watahiniwa 544 (0.64%) hawakufanya mtihani.

Kwa Watahiniwa wa Kujitegemea, kati ya watahiniwa 10,412 waliosajiliwa, watahiniwa 9,586 sawa na asilimia 92.07 walifanya mtihani na watahiniwa 826 sawa na asilimia 7.93 hawakufanya mtihani.

MATOKEO YA MTIHANI
Jumla ya watahiniwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2022 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 40,907 sawa na asilimia 99.51 wakati wavulana waliofaulu ni 52,229 sawa na asilimia 98.55. Mwaka 2021 watahiniwa waliofaulu walikuwa 87,043 sawa na asilimia 99.06.

Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 84,404 sawa na asilimia 99.87 ya waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 37,384 sawa na asilimia 99.91 na wavulana ni 47,020 sawa na asilimia 99.83. Mwaka 2021 Watahiniwa 79,596 sawa na asilimia 99.62 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo.

Idadi ya Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 8,732 sawa na asilimia 91.11. Mwaka 2021, Watahiniwa wa Kujitegemea 7,447 sawa na asilimia 93.45 walifaulu mtihani huo.

UBORA WA UFAULU
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 83,877 sawa na asilimia 99.24 wamefaulu katika Daraja la I hadi III wakiwemo wasichana 37,170 sawa na asilimia 99.34 na wavulana 46,707 sawa na asilimia 99.16.

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Jumanne Julai 5, 2022 limetangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Sita na kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 99.87.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*