WAZIRI WA FEDHA AIPONGEZA BRELA KWA HUDUMA BORA



 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto) akimkabidhi tuzo ya udhamini wa Kongamano la 14 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa (kulia), Desemba 12, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa, Arusha (AICC).

 

Waziri wa  Fedha   Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba(Mb), ameipongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.    


Mhe. Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo leo tarehe 12 Desemba, 2023 wakati alipotembelea banda la BRELA lililopo nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), linapofanyika Kongamano la 14 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi  na Ugavi.


Dkt. Nchemba amesema amefurahishwa na huduma nzuri inayotolewa na BRELA ambayo ameilezea kuwa itaongeza idadi kubwa ya wadau watakaorasimisha  biashara zao.


“Nimefurahishwa sana na huduma nzuri inayotolewa na BRELA, hivyo basi  wafanyabiashara na wawekezaji ambao bado hawajarasimisha biashara zao ni vyema wakafuata taratibu sahihi za kusajili,” amesema Mhe. Dkt. Nchemba.


Aidha, Waziri wa Fedha  ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha, kuchangamkia fursa hiyo ya kurasimisha biashara zao na kufika katika banda la BRELA ili kupata huduma za urasimishaji.


Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa  amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa, Taasisi  itaendelea kutoa huduma bora wakati wote, lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wadau hawakumbani na vikwazo vya kibiashara.  


Kongamano la 14 la mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lililofunguliwa leo tarehe 12 Decemba, 2023 litahitimishwa  tarehe 14 Desemba, 2023 jijini Arusha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA