WAZIRI KITILA AELEZEA MAFANIKIO MAKUBWA WIZARA YA MIPANGO, UWEKEZAJI




 NA JOHN BANDA, DODOMA

WAZIRI wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo leo A[rili 17,2024 amekutana na waandishi wa Habari jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaeleza kuhusu Nchi ilipotoka ilipo sasa na inapoelekea kwa kutaja mambo kadhaa ya kujivunia yakiwepo maendeleo hasa wakati huu tunapoelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano


“Tunapopima mafanikio hatua ya kwanza katika miaka 60 ya muungano ni uhai wa muungano wetu, Kitu cha pili kuhakikisha kwamba muungano huu unadumu na kulinda amani, utulivu na mshikamano”, amesema


Aidha amesema Hatua ya tatu ni kujipima katika maendeleo kwa kuwa na usalama wa chakula. Wakati ule tumeungana, usalama wa chakula ulikuwa asilimia 60 huku lengo la nchi ni kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na kuwa na akiba. Kwa sasa nchi ina usalama wa chakula kwa asilimia 124.


Hatua ya nne ni kujipima katika maendeleo ni ustawi wa watu na nchi kwa kuangalia mambo ya msingi ya kibinadamu ikiwemo chakula, mavazi na malazi ambayo nayo tumepiga hatua kubwa.


Wakati tunapata Uhuru, umri wa kuishi kwa Mtanzania ilikuwa wastani wa miaka 32, mwaka 2000 umri wa kuishi ukasogea hadi wastani wa miaka 52. “Tamaa yetu ifikapo mwaka kesho 2025 wastani wa kuishi uwe miaka 68. Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, ilionyesha wastani wa kuishi ni miaka 66”, amesema


Mambo matatu ya kufanya kukuza ustawi wa binadamu ni kumpa binadamu elimu ili aweze kuishi vizuri ambapo mwaka 2000 nchini Tanzania, kiwango cha kuandikisha wanafunzi kilikuwa asilimia 69. Kwa malengo tuliyojiwekea kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025, ni kufikia asilimia 100 ya uandikishaji wa wanafunzi ambapo hadi sasa tumevuka malengo, tupo asilimia 108.5.


Kuhusu suala la kwenda sekondari, mnamo mwaka 1964 ilikuwa asilimia 5, mnamo mwaka 2000, watoto waliofanikiwa kufika sekondari kutoka shule za msingi ilikuwa chini ya asilimia 20. Lengo letu ifikapo mwaka 2025, tuwe tumefika asilimia 48. Kwa takwimu za hivi sasa, tupo asilimia 70.


Dira ya Maendeleo ya Taifa inayokuja, tutahitaji elimu ya msingi Tanzania iwe kwa Watanzania wote na wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.


Eneo lingine katika kukuza ustawi wa binadamu ni afya hasa kwenye eneo la mama na mtoto, na la tatu ni maji ambapo wakati tunapata uhuru, uwepo wa maji vijijini ulikuwa chini ya asilimia 15 na mwaka 2000 ilikuwa asilimia 32. Kwa sasa ni asilimia 77.


Nchi inahitaji uwepo wa uchumi, kukua kwa uchumi ni nyenzo muhimu. Ili nchi ione inapiga hatua ni lazima iangalie uchumi unaendaje.


Tanganyika na Zanzibar ziliungana Aprili 26, 1964 ambapo kila mwaka maadhimisho ya Muungano huo hufanyika kila tarehe na mwezi huo kama ilivyo kwa mwaka huu ambao kilele chake kitafanyikia Uwanja wa Uhuru jijin Dar eslaam. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE