WAZIRI MKUU MAJALIWA AZIAGIZA HALMASHAURI KUZIJENGEA UZIO SHULE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri nchini kutumia sehemu ya mapato yao ya ndani kujenga uzio katika shule kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na rasilimali.

Ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari na za Msingi kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Desemba 12, 2024.

Naye Rais wa Chama hicho, Denis Otieno  ametoa shukrani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuingiza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya shule nchini, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ya elimu nchini.


Kassim Majaliwa akihutubia katika mkutano huo.

Wajumbe wa mkutano mkuu ambao ni  wakuu wa shule za sekondari na za msingi nchini wakiwa makini kumsikiliza Waziri Mkuu.







 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akijadiliana jambo na Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO

AHMED ALLY KULIPA BIL. 10 KWA KUIKASHIFU YANGA