Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa Mamlaka hiyo imewezesha zaidi ya kaya masikini 6000 zimeunganishiwa maji kwa gharama nafuu ya sh. 30,000 kwa Kila kaya.
Pamoja na mambo mengine, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Machi 14, 2025, kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Mhandisi Rujomba amesema kuwa AUWSA imevunja rekodi kwa kutoa huduma ya maji kwa asilimia 99 badala ya asilimia 95 inayotakiwa kufikiwa ifikapo 2025 kwa mujibu wa utekekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments