✍️
Taarifa kutoka nchini Misri zinaripoti taarifa rasmi kutoka Shirikisho la Vilabu nchini Misri kuwa Zamalek imepewa ushindi wa mabao matatu na alama tatu baada ya Al Ahly kutotokea uwanjani kwa kutumia kifungu cha 4(17) kwenye Sheria na Kanuni za Mashindano.
.
Sambamba na hilo Al Ahly, wamekatwa alama tatu (zitachukuliwa mwishoni mwa msimu) huku pia wakiagizwa kulipa gharama zote za kibiashara pamoja na gharama za Warusha matangazo sambamba na gharama nyingine za ziada kwa mujibu wa kifungu cha 8(17).
.
Licha ya hivyo Al Ahly wamepeleka malalamiko yao kwa Kamati ya Olympic nchini humo ambapo Shirikisho la soka Misri likisubiri majibu ya sakata hilo.
.
Comments