Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Bi. Latifa M. Khamis, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 13, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
MAFANIKIO
YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA MWAKA 2023/2024 NA 2024/2025
Katika
kipindi hiki, TanTrade imefanikiwa kupanua masoko, kusaidia biashara za
Tanzania kupata fursa za kimataifa, kujenga uwezo wa wafanyabiashara wadogo na
wa kati, na kuboresha mifumo ya upatikanaji wa taarifa za biashara.
1.1
Kuratibu na Kusimamia Mifumo ya Soko la Ndani
Katika eneo hili, Mamlaka imetekeleza mambo
yafuatayo;
a.
Uratibu wa DITF ambao ulipelekea mafanikio yafuatayo kwa kipindi cha mwaka
2020/21 -2023/24:
i.
Washiriki wa ndani wameongezeka kutoka 2,926 hadi 3,503, huku washiriki wa
nje wakiongezeka kutoka 76 hadi 451.
ii.
Nchi zinazoshiriki zimeongezeka kutoka 17 hadi 28.
iii.
Watembeleaji wa maonesho wamefikia zaidi ya 300,701.
iv.
Ajira za muda mfupi zimeongezeka kutoka 11,200 hadi 11,869.
v.
Mauzo ya papo kwa papo yamefikia shilingi bilioni 3.62.
vi.
Fursa za mauzo kupitia maonesho zimefikia thamani ya shilingi bilioni 25.16
vii.
Mikataba ya kibiashara yenye thamani ya shilingi bilioni 176 ilisainiwa,
ongezeko kubwa kutoka shilingi bilioni 5.6
b.
Hati za
Makubaliano (MoU) zenye thamani ya shilingi bilioni 17 zilisainiwa kupitia Maonesho ya Biashara ya Kimataifa
ya China (CIIE) 2023/24
c.
Expo 2020
Dubai
i.
Kusainiwa
kwa (MoU) 36 za makubaliano zenye thamani ya Dola Bilioni 7.49 (Tshs. Trilioni
17.35).
ii.
Ajira
200,000 zilipatikana.
iii.
Washiriki
640 wa Kitanzania walihudhuria.
iv.
Watembeleaji 928,469 kutoka nchi mbalimbali
duniani walitembelea sehemu ya maonesho ya Tanzania (Tanzania Pavillion).
d.
Maonesho ya Mbogamboga Expo
Doha, 2023/24
i.
Kampuni 13 zilishiriki na kufanikisha mauzo ya papo
kwa papo ya shilingi milioni 370.
ii.
Fursa za mauzo za shilingi milioni 125 zilifunguliwa
kupitia mazungumzo ya kibiashara.
iii.
Kampuni za Qatar zilionesha nia ya kuwekeza katika
usindikaji wa chakula na usimamizi wa taka.
e.
Maonesho ya Biashara ya Afrika
(AfCFTA Exhibitions on Intra-Africa Trade) ya mwaka 2023 ambapo: -
i.
Mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya TZS bilioni 2.17 yalifanyika.
ii.
Mikataba
ya biashara yenye thamani ya TZS bilioni 17 ilisainiwa.
1.1
Kutoa
mafunzo na ushauri kwa sekta binafsi hususani Wafanyabiashara
TanTrade
imeendelea kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuwawezesha
kushindana katika masoko ya ndani na nje kupitia mafunzo ya biashara.
a. Programu 37 za mafunzo zimeratibiwa, zikihusisha
wafanyabiashara 3,556. Mada zilizofundishwa katika kipindi cha miaka minne ni pamoja na:
i.
Usimamizi
na uendeshaji wa biashara (washiriki 922)
ii.
Mbinu za
kufikia masoko ya ndani na nje (washiriki 630)
iii.
Taratibu
za kuuza nje na uelewa wa mfumo wa taarifa za biashara (washiriki 253)
iv.
Mafunzo
kwa wafanyabiashara wa mipakani (washiriki 51).
b. Katika
kipindi cha miaka minne mafanikio yafuatayo yalipatikana kupitia Kliniki za
biashara;
i.
Jumla ya wafanyabiashara 3,256 walihudumiwa
kupitia kliniki zilizofanyika katika maonesho na mikutano ya kibiashara.
ii.
Jumla ya changamoto 1,324 ziliwasilishwa, ambapo 1,298 zilitatuliwa, na 26 zipo katika hatua za utekelezaji,
hususan zinazohusiana na mitaji na vibali vya biashara.
iii.
Kampuni 482 zilipatiwa
msaada wa usajili kupitia taasisi wezeshi kama BRELA, BPRA, na TRA, na biashara mpya zilianzishwa.
iv.
Kampuni 137 zilisaidiwa
kupata ushauri alama za ubora, vifungashio vinavyokidhi viwango vya soko la
kimataifa, na mbinu za kuongeza thamani ya bidhaa.
v.
Wafanyabiashara 238 waliunganishwa
na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi kupitia mikutano ya B2B na B2G, ambapo
biashara za bidhaa kama asali, mazao ya
nafaka, mbogamboga, na viungo zilifanikishwa.
vi.
Wafanyabiashara 312 walipatiwa
mafunzo kuhusu mbinu bora za biashara,
taratibu za forodha, na miongozo ya kodi kupitia TRA.
Comments