FALSAFA NA UTAMADUNI WA KOCHA MPYA WA YANGA


Kocha mpya wa Yanga Romain Folz ana haiba kali ya kusema ukweli mara moja sio mtu wa kupepesa macho kitu ambacho kinamfanya aonekane mkali.Pia Romain Folz  ni kocha ambaye anaamini sana kwenye mpira wa kisasa (modern tactics).


Falsafa ya Romain Folz  ni kucheza mpira wa kasi na pasi fupi fupi na utawala wa mechi (pitch Supremacy).Msingi wa Falsafa ya Romain Folz ni


1.Kucheza kwenye mfumo wa 4-3-3 defending.

Kwenye mfumo wa 4-3-3 defending Romain Folz msisitizo wake mkubwa uko hapa


1.Washambuliaji watatu wa kwanza pale mbele kuanza kuweka presha kwenye mpira kwenye mstari wa kwanza wa mpinzani wakati timu haina mpira.


2.Kuitawala mechi kupitia katikati (Midfield Control)

Romain Folz kwenye mfumo wa 4-3-3 siku zote viungo watatu anapenda wawe na mamlaka ya kuitawala mechi katikati ya uwanja.Romain Folz anapenda viungo watatu kwenye mstari wa pili kwenye 4-3-3 wawe wapiga pasi wazuri,uwezo wa kuitoa timu chini kwenda juu.


3.Mabeki wa pembeni wahusike kwa ufasaha kwenye kushambulia.


Romain Folz anaamini sana timu kushambulia kupitia kwenye mapana ya uwanja.RomainFolz kwake mafullbacks ni sehemu ya kumfungua mpinzani kutokea pembeni.


4.Kushambulia na kujilinda kwenye kipindi cha  haraka cha mpito (Quick Transition)


Romain Folz anapenda timu yake ikipoteza mpira lazima iwe na uwezo wa ku react haraka kwenye kuzuia pia ikopora mpira iwe na uwezo kushambulia haraka haraka kwenda kwenye sanduku la mpinzani.


5.Mabeki wa kati wawe na uwezo kucheza mpira (Ball Playing Defenders).

Romain Folz anapenda sana timu itoke nyuma kwa pasi sahihi hasa kwa mabeki wawili wa kati.Hivyo sifa ya mabeki wa kati kwenye falsafa yake lazime wawe wana uwezo wa kupasia mpira vizuri kwa nyakati zote.


Romain Folz Principle 

1.Possesion Based Football 

2.High Pressing 

3.Quick Transition


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

DIARRA KIPA BORA TANZANIA