Marehemu baba yetu alifariki mwaka 2006. Wakati huo, mimi nilikuwa darasa la sita. Nilipomaliza darasa la saba mwaka uliofuata (2007), nilifaulu vizuri na nilipata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Lakini kaka yetu mkubwa, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa amefungua maduka mawili, alinieleza kuwa niachane na shule ili niende kusaidia kuuza mojawapo ya maduka yake na kuishi pamoja na mke wake.
Kwa kuwa kaka ndiye aliyekuwa kila kitu katika familia yetu kwa wakati huo, sikuwa na namna zaidi ya kukubali. Nikaanza kuuza duka hilo, na nilikaa hapo kwa miaka miwili. Duka likakua sana hadi tukalazimika kuunganisha fremu mbili kuwa duka moja, kwa idhini ya mwenye fremu.
Baada ya muda tukawa wauzaji watano ndani ya duka hilo moja. Mauzo yakawa makubwa sana – hadi kufikia milioni 30 kwa siku π️. Jambo la kushangaza, duka lilionekana la kawaida tu kwa nje, lakini lilikuwa na wateja wengi kupita maelezo.
Baadaye kaka alinipangia duka lingine la kuuza dawa (pharmacy), ambalo lilikuwa linahudumia jumla na rejareja. Mpaka leo hii bado nipo hapo. Hili nalo ni duka kubwa tupo wauzaji sita na siku nyingine mauzo hufika hadi milioni 400 kwa siku ππ°.
Katika duka hili, mimi ndiyo msimamizi mkuu. Kaka amenikabidhi mamlaka yote – nikitaka kununua gari, nanunua π. Nikitaka kujenga nyumba, najenga π .
Kabla hajanikabidhi duka hili rasmi, kaka alinisisitiza jambo moja muhimu sana: nisifungue duka kabla ya saa mbili asubuhi, na lazima nifunge kabla ya saa nne usiku⏰. Kila tukikutana hata kwenye starehe au vikao, alikuwa hatasahau kukumbusha hilo kwa msisitizo mkubwa. Kwa wakati huo, nilidhani ni mambo ya ushirikina wa kawaida tu kama walivyo wafanyabiashara wengi wakubwa.
Sasa, siku ya Jumatatu iliyopita, kuna wateja waliokuwa wametoka mkoani walinipigia simu saa 12 alfajiri wakisema wapo ofisini wanahitaji kufunga mzigo haraka. Bila kuwaza sana, nikawasha gari na kuelekea kazini mapema.
Nilipofika na kufungua mlango, nilimkuta marehemu baba yangu mzazi ameketi kwenye kiti ambacho huwa nakaa mimi kila siku π¨. Nilishtuka ghafla hadi nikakimbia nje hata wale wateja walinishangaa. Nilikuwa natetemeka, waliponiuliza kuna nini, sikuweza hata kutoa jibu.
Nilijikaza nikarudi kuchungulia tena, sikuona mtu yeyote mle ndani. Nikarudi nje tena, nikaanza kuangaza huku na kule bado nikiwa nimeshtuka sana π.
Wakati bado nipo pale nje, nikiwa nimechanganyikiwa, ghafla nikamwona kaka anakuja kwa kasi huku akiwa na hasira kali sana. Nikamkimbilia kabla hajashuka kwenye gari na nikamwambia kilichotokea.
Badala ya kuelewa, alinipiga vibaya sana, akanitukana na kuniambia niondoke kabisa na isiwe tena na mimi kukanyaga dukani π’.
Mpaka sasa sijamwambia mtu yeyote kuhusu kilichotokea. Lakini leo, kaka amenipigia simu akaniambia kesho niende dukani. Moyoni, roho yangu imejaa hofu kubwa sana π. Kijijini kulikuwa na maneno kwamba kaka ndiye alimhangaisha baba kwa kafara, ila tulikuwa hatuamini... sasa nahisi kuna ukweli ndani yake.
Nawaza kuwaambia ndugu na hata mama, lakini naogopa sana. Naogopa hata kuonana na kaka, na natamani nirudi kijijini. Lakini kila nikifikiria, naona picha ya kaka akinifanyia jambo baya.
Na tangu siku ile ya Jumatatu, kila nikilala ninaota kaka akinikimbiza kwenye msitu mkubwa wa miti mikubwa, nikiwa napiga kelele lakini hakuna wa kunisaidia π²π’.
Hii ya kuniita kesho dukani inanipa wasiwasi mkubwa nahisi kama ana mpango wa kunidhuru kwa kuhisi labda nitamwaga siri hii kwa wengine.
Naandika haya nikiomba msaada wa mawazo yenu... Maana kila nikiwaza nifanye nini, naishia kuhisi kama nitakuwa nakosea π.
Comments