Viongozi wa Benki ya NMB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, CPA. David Carol Nchimbi,(Kulia) wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC) jijini Dodoma, wakifuatilia kwa makini hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Uzinduzi huo umefanyika leo chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi.
Benki ya NMB, kama mshirika mkuu wa maendeleo ya kiuchumi nchini, imeonesha dhamira yake ya kuunga mkono utekelezaji wa Dira hii mpya inayolenga kuifikisha Tanzania katika hatua za juu za maendeleo jumuishi, shindani na endelevu ifikapo mwaka 2050.
Comments