TABIA ZA WANANDOA ZINAZOHARIBU UCHUMI WA FAMILIA NA KUWAGOMBANISHA

1. KUFICHA HELA
 Wanandoa wengi hufanya mambo kwa siri. Kuficha mapato, kukopa hela kwa siri na kuficha, kusaidia ndugu kwa siri au kufanya manunuzi kwa siri.

2. KUKOSA MIPANGO
Kuna wanandoa wanafanya mambo kwa kujisikia na si kwa mipango. Wakijisikia kwenda out wanaenda, wakijisikia kununulia watoto nguo wananunua, wakijisikia kusaidia wazazi wanasaidia yaani hawana mpango wa muda mfupi wala muda mrefu. Pesa inapokosa mwelekeo maalumu na mipango hupotea. 

3. MATUMIZI KUZIDI MAPATO
Maisha ya kuwaonesha wengine kuwa una uwezo kwa kulazimisha kununua magari wasiyo, nguo za kifahari, kutoa michango mikubwa kuliko uwezo, hupelekea wanandoa wengi kushindwa kufanya mambo ya maana

4. KUTOWEKA AKIBA YA DHARULA
Maisha yana mambo mengi ambayo hayatarajiwi. Wanandoa wanaposhindwa kujiwekea akiba ya dharula linapotokea jambo la ghafla hujikuta wanavurugikiwa na mara nyingine kuleta magomvi.

5. KUSIKILIZA MATAKWA YA NDUGU
Ni vizuri kusaidia ndugu lakini msipokuwa makini ndugu wanaweza kuwaburuza na kujikuta hamfanyi mambo yenu bali matakwa ya ndugu. Kuna ndugu hulazimisha wadogo zao kufanya mambo fulani kwa ajili ya ukoo hata kama hayakuwemo kwenye bajeti zao.

6. MASHINDANO BADALA YA USHIRIKIANO
Kuna wanandoa wanashindana vipato badala ya kushirikiana kukusanya ili kufanya mambo ya maemdeleo kwa pamoja

7. KUKOSA ELIMU YA FEDHA 
Vijana wengi hukimbilia ndoa bila kupata elimu kuhusu mambo ya fedha. Baada ya harusi ndipo huanza kukutana na hali halisi kwani katika familia maisha huwa tofauti na walivyozoea wakiwa peke yao. Wengi huogopa kuongea maswala ya pesa wakati wa uchumba kwa kuogopa kuonekana wabinafsi au wanapenda pesa matokeo yake baada ya ndoa wanaanza kugombana.

8. KUTEGEMEA CHANZO KIMOJA
Kutegemea kipato cha mwanandoa mmoja kwa dunia ya leo ni hatari sana. Mmoja akipoteza kazi au biashara kuyumba au akifariki familia nzima inapita misukosuko. Ni vizuri kukawa na vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja ili kusaidiana.

9. KUTOMHESHIMU MUNGU KWA MALI ZAKO
Kutomheshimu Mungu kwa mali uhufunga mlango wa msaada na ulinzi wa kiungu dhidi ya mapato ya familia. 

10. KUKOSA MGAWANYO WA MAJUKUMU YA KIUCHUMI
Ni vizuri wanandoa wakakakubaliaba nani atalipia nini kila mwezi. Haitakiwi mwanandoa mmoja kubeba mzigo wa kiuchumi peke yake..

11....???


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE....

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

RAIS WA BURKINA FASO ATANGAZA DIRA YA KUUNDA MUUNGANO WA MATAIFA YA AFRIKA (UNITED STATES OF AFRICA).