MBEYA, NJOMBE, SONGWE WAPIGA MAGOTI KUMUOMBEA KURA ZA KISHINDO DKT. SAMIA

BAADHI ya viongozi na wagombea ubunge  katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamekuwa wakitumia utaratibu wa kupiga magoti mbele ya wananchi kumuombea kura Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‎Ishara hiyo ya kuonesha unyenyekevu kwa wananchi imekuwa ikijitokeza katika baadhi ya mikutano ya kampeni ya Chama hicho kama ilivyojitokeza katika mikoa ya Mbeya, Songwe,  Njombe na Iringa.

‎Katika Mkoa wa Mbeya kwenye mkutano wa kampeni katika Mji wa Mbalizi, Mbunge Mteule wa Viti Maalumu kupitia Wanawake wa Mkoa  huo, Suma Ikenda Fyandomo alipiga magoti mbele ya wananchi akiwaomba na kuwasihi kukumbuka siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025 kumpigia kura za kidhindo Dkt . Samia, wabunge na madiwani wa CCM.

Kitendo hicho ambacho kwa jamii na makabila mengi ya mikoa ya Nyanda za Juu kusini kinaonesha utii na unyenyekevu, kilijirudia kwenye mkutano wa kampeni katika Mji wa Makambako Septemba 6, 2025, ambapo  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga naye alipiga magoti kwa lengo hilo hilo la kumuombea kura Dkt. Samia na CCM  kwa jumla.



Septemba 7,  2025 kitendo hicho kimejitokeza tena kwenye mkutano wa kampeni za Dkt. Samia  katika Uwanja wa Samora Iringa Mjini, kwa wagombea ubunge wateule wa viti maalumu kupitia wanawake wa Mkoa huo, Rose Twelve na Nancy Nyalusi nao wakipiga magoti kwa kusudi hilo hilo la kumuombea kura za kidhindo, Dkt. Samia , wabunge na madiwani.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga.

Nancy Nyalusi 
Rose Twelve

Mbunge Mteule wa Viti Maalumu kupitia Wanawake wa Mkoa  huo, Suma Ikenda Fyandomo


 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MSIMAMIZI MKUU

KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV

0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA