DKT. SAMIA AAHIDI KUANZISHA VITUO VYA KUKODISHA MATREKTA KWA BEI NAFUU



 MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuanzisha vituo vya ukodishaji trekta nchini

‎Amesema trekta hizo na zana zingine za kilimo  zitakuwa zinakodishwa kwa wakulima kwa bei nafuu, yaani nusu ya bei ya matrekta ya watu binafsi.

‎Ametoa ahadi hiyo katika mkutano mkubwa wa kampeni za CCM uliofanyika Leo Septemba 7, 2025 kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

‎Aidha, Rais Dkt. Samia ameendelea kuelezea kuwa endapo Wananchi watampatia ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, Serikali yake itaendelea kutoa ruzuku ya mbolea na pembejeo kwa wakulima nchini.

‎Amesema kuwa kitendo cha Serikali kutoa ruzuku katika mbolea kumeleta tija ya uzalishaji wa mazao na hasa mahindi ambayo yameifanya Tanzania kushika nafasi ya pili Afrika kwa kuzalisha zaidi ya tani milioni 10.

‎Ameahidi pia kuendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu ya barabara, afya, maji na elimu.

‎Licha ya kujinadi, Rais Dkt. Samia ametumia fursa hiyo kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho.

‎Amehitimisha kampeni katika Mkoa wa Iringa baada ya Jana kujinadi eneo la Nyororo na Mafinga wilayani Mufindi pamoja na Kalenga Wilaya ya Iringa vijijini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-

RC KIHONGOSI AELEZA MAFANIKIO LUKUKI MKOA ARUSHA

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO