Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku Hospitali za Serikali kuzuia miili ya waliofariki dunia inayodaiwa.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Ndege wa zamani Mwanjelwa jijini Mbeya Septemba 4, 2025 na kwamba Serikali itaandaa mfumo maalumu wa ndugu kulipa deni kabla au baada.
Aidha Dkt. Samia amesema kuwa Serikali itatenga fedha za mfuko maalumu wa kugharamia matibabu ya vipimo maalumu ya kibingwa kwa wasio na uwezo.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments