Mwenyekiti wa machifu wa Mbeya Vijijini, Shayo Masoko amewaomba machifu wa nchi nzima kuungana kwa kutumia mila na tamaduni zao kuwalaani wanaotumia mitandao kumchafua Rais Samia Suluhu Hassan na kutaka kuvuruga amani ya Nchi.
Ameyasema hayo alipokaribishwa kutoa neno wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Mbalizi, Mbeya Vijijini leo Septemba 4, 2025.Machifu zaidi ya 270 wa Mbeya Vijijini wameshiriki kwenye mkutano huo kumuunga mkono mgombea huyo kwa kuahidi kumpigia kura.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments