MIKOA NYANDA ZA JUU KUMPATIA DKT.SAMIA USHINDI WA AJABU- CHONGOLO


KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Songwe, Daniel Chongolo amemuahidi Mgombea Urais wa Chama hicho, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini itampatia ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.


Chongolo ambaye sasa ni Mgombea ubunge wa jimbo la Makambako mkoani Njombe na mratibu wa kampeni za CCM  wa Kanda hiyo, ametoa ahadi hiyo alipokaribishwa kusalimia Wananchi katika mkutano wa kampeni wa chama hicho eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe Septemba 3, 2025.


Ahadi kama hiyo ameitoa pia katika mkutano wa awali uliofanyika katika MJi wa Tunduma. Ametaja mikoa hiyo kuwa ni Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa.


Naye Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye pia ni mratibu wa kampeni wa mikoa ya Kanda ya Kati ya Dodoma, Singida na Tabora, Dkt. Bashiru Ali, aliahidi ushindi mkubwa wa CCM kwa mikoa hiyo.


DKT. Samia ambaye Mgombea Mwenza wake ni Dkt. John Emmanuel Nchimbi amemaliza Kampeni zake mkoani Songwe na kesho Septemba 4,2025 atafanya kampeni katika Mji wa Mbalizi na Mbeya Mjini katika Uwanja wa Ndege wa zamani.


Septemba 5, 2025, ataendeelea na kampeni

zake katika Mkoa huo ambapo asubuhi atafanya mkutano wilayani Rungwe na baadaye wilayani Mbarali katika miji ya Igawa na Ubaruku. 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MSIMAMIZI MKUU KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI