Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amelikubali ombi la kuupandisha hadhi Mji mdogo wa Mbalizi kuwa Halmashauri ya Mji.
Amesema kuwa endapo mchakato ndani ambao umeanza ukifikishwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) basi wao kama serikali wataangalia ni jinsi gani ya kuipandika hadhi Mbalizi kuwa Halmashauri ya Mji.
Dkt. Samia ametoa majibu hayo liyopokelewa kwa shangwe na wananchi wa mji huo baada ya kuombwa na Mbunge Mteule wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Patali Shida Patali wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea huyo urais uliofanyika leo Septemba 4, 2025 kwenye viwanja vya Mlima Reli Mbalizi mkoani Mbeya.
Comments