1. Ishinde sauti yako ya ndani inayokukosoa mara kwa mara.
Nafsini mwako kuna sauti ambayo inakwambia mara kwa mara hauwezi kufanya jambo fulani. Iepuke sauti hiyo kwasababu itakufanya ubakie kama ulivyo siku zote.
2. Epuka mtego wa kujilinganisha na watu wengine.
Kataa kabisa kujifananisha na watu wengine, wewe ni wewe lazima uwe wa tofauti kwasababu kila mtu amepatiwa karama na kipaji chake. Usifanye mambo kwa mashindano au kujifananisha bali mshindani wako awe ni wewe mwenyewe kwa kuhakikisha unakuwa tofauti na ulivyokuwa jana.
3. Sherehekea kila hatua ndogo ya mafanikio yako.
Kila wakati unapofanikiwa kwenye jambo fulani hakikisha unajipongeza kujipa hamasa ya kufanya jambo kubwa zaidi.
4. Kuwa na fikra au mawazo chanya.
Hakikisha unajaza fikra nzuri kichwani mwako na sio mambo mabaya kama vile kuwaza magonjwa,vifo,kurogwa au vitu vyovyote hasi ambavyo vinakufanya uishi maisha ya hofu ushindwe kufanya maendeleo. Jitamkie na jiwazie mambo mazuri wakati wote!
5. Jifunze kuongea kwa utaratibu.
Kataa tabia ya kuongea kwa kupayuka, jifunze kuongea kwa upole na ustaarabu. Hiyo ndiyo tabia ya watu wakuu Duniani.
6. Kila wakati vuta picha ya Mafanikio yako.
Wakati unapambana na maisha, vuta picha kama mtu aliyefanikiwa tayari na kufika mbali. Ukiwa unajitafuta jione tayari wewe ni mtu mkubwa, ona makampuni unayomiliki, biashara unazomiliki,majumba na magari unayomiliki kichwani mwako. Hiyo ndiyo Siri ya watu waliofika mbali, kichwani hujiona washindi hata kabla hawajashinda.
7. Kuwa mkarimu kwa wengine.
Jitahidi kuishi maisha ya kutoumiza wengine. Utafika mbali sana kwasababu unayeishi naye vizuri leo hujui utakutana naye wapi kesho na atakupa msaada kwenye jambo gani.
8. Kubali kuwa wewe sio mkamilifu.
Usitake kuwa mkamilifu kwasababu kitu hicho HAKIWEZEKANI. Mkamilifu ni Mungu pekee.
9. Usijilaumu unapofanya makosa bali JIFUNZE kupitia makosa hayo.
Unapofanya makosa,usijihukumu bali hakikisha haurudii kosa hilo.
10. Tafuta muda wa kuwa pamoja na watu ambao unawapenda na wanakufanya ujihisi Vizuri.
Kila wakati tenga muda wa kufurahia na watu uwapendao(kuzungumza nao, kula chakula nao au kucheza nao). Hii itakupa hamasa ya kupambana zaidi kwasababu nyuma yako Kuna watu ambao wanakutegemea lakini pia utakuwa na afya nzuri ya Kiakili.
11. Amini kuwa mabadiliko yanawezekana.
Amini kila jambo linawezekana kubadilika au unaweza kulibadilisha. Nyakati ngumu za maisha unazopitia hazidumu milele. Watu waliofanikiwa wanabuni vitu vipya kila wakati kwasababu wanaamini kwenye mabadiliko.
12. Kamwe usiogope kuthubutu.
Kila wakati usiogope kuanzisha kitu kipya kwasababu ya hofu ya kushindwa. Watu waliofanikiwa hawaogopi kuthubutu ( kutake risk).
Je, unafikiri ni kitu gani kipya umejifunza kwenye somo hili unaamini ukikizingatia kitabadilisha maisha yako?
Mwalimu Hakika
Kigoma, Tanzania.
Comments