Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Mhe. Domittien Ndayizeye, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Burundi na Mkuu wa Kamisheni ya Jukwaa la
Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa
Makuu (ICGLR).
Mazungumzo yao yamehusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Jopo la Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Ukanda wa Maziwa Makuu lipo nchini kufuatilia hatua za maandalizi ya uchaguzi huu wa saba tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ikiwa ni kielelezo cha uimara wa demokrasia nchini. 🇹🇿🗳️








Comments