DKT.SAMIA NITAHAKIKISHA NAKUSAIDIA KWA NGUVU, AKILI, MAARIFA NA UAMINIFU - DKT. NCHIMBI

‎Mgombea mwenza wa Urais katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema kuwa kwa imani pekee  aliyoionesha kwake Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia kuwa namna pekee anayoweza kuilipa ni kumsaidia kwa nguvu, akili, maarifa na uaminifu ili ndoto na maono yake na utekelezaji wa ilani  ya CCM (2025/30) ufanyike kwa mafanikio makubwa katika miaka mitano ijayo.

‎"Nakushukuru sana Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama chetu cha CCM kwa imani yako kubwa kwangu kwa kunipendekeza kuwa msaidizi wako mkuu, miaka minne iliyopita uliniteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misiri, badae ukanipendekeza  kupitia vikao vya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM na sasa umeniamini katika nafasi ya Mgombea Mwenza"

‎"..ndani ya miaka minne umeonesha imani yako kwangu kwa kunipa nafasi muhimu ndani ya Taifa letu na ndani ya CCM.."

‎"..nakuhakikishia kuwa imani uliyoonesha, namna pekee ninayoweza kuilipa ni kukusaidia kwa nguvu, akili, maarifa na uaminifu ili ndoto na maono yako na utekelezaji wa ilani yetu ya CCM (2025/30) ufanyike kwa mafanikio makubwa katika miaka mitano ijayo."

‎"Watanzania katika sehemu zote tulizopita wameridhika na utekelezaji wako wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 kwa kishindo na wametutuma tukueleze kuwa kesho watakupa kura nyingi za ushindi wa kishindo"

‎"..hilo linatokana na utendaji kazi wako katika Serikali ya awamia ya sita unayoiongoza inayotakana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).."

‎Hayo yamesemwa na Mgombea mweza wa Urais katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Ndugu. Dkt. Emmanuel John Nchimbi, wakati akizungumza mbele ya umati wa Wananchi wa Mwanza na maeneo ya karibu katika mkutano wa kuhitimisha Kampeni za Uchaguzi za CCM, leo tarehe 28 Oktoba 2025.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA