HITIMISHO LA KAMPENI ZA CCM NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

 JUMATATU, 27.10.2025:
Kwa kuzingatia maombi ya wananchi na viongozi wao, Prof Muhongo atafanya hitimisho la kampeni zake kesho, Jumatatu, 27 Okt 2025 kama ifuatavyo:

Mkutano I:
Saa 7 mchana hadi saa 9 alasiri.
Kata ya Bugwema
Kijijini Kinyang'erere. 

Mkutano II:
Saa 10-12 jioni.
Kata ya Bugoji
Kijijini Bugoji.

JUMANNE, 28.10.2025
Jijini Mwanza
Kushiriki hitimisho la Ki-Taifa

KAMPENI ZIMEKAMILISHWA IFUATAVYO:

Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374

Kampeni zimefanyika ifuatavyo:
1. Kata 21
Mikutano ya ndani kwa Kata zote

2. Vijiji 68
Mikutano ya hadhara kwa Vijiji vyote

3. Visiwa 3 vya Ziwa Victoria 
Mikutano ya hadhara ilifanywa kwenye Visiwa vya Rukuba, Iriga na Kagongo

4. Vitongoji vikubwa 6
Vitongoji hivi ni vikubwa vyenye wakazi wengi. Mikutano ya hadhara ilifanywa huko.

5. Kampeni ya nyumba kwa nyumba
Kampeni hii inayoendelea hadi tarehe 28.10.2025 inafanywa ndani ya Kata zote 21. Viongozi wa Chama wa Mashina, Matawi na Kata wanashirikishwa vizuri

WAJUMBE WA TIMU YA KAMPENI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI 

1. Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya
2. Sekretariati ya Ofisi ya Chama Wilaya
3. Viongozi wa Chama wa ngazi zote kwenye maeneo yao
4. Mgombea Ubunge, Prof Sospeter Muhongo 
5. Wafanyakazi wa Ofisi ya Mbunge (Prof S Muhongo)
6. Baadhi ya Watiania (CCM) kwenye nafasi ya Udiwani
7. Watiania (CCM) kwenye nafasi ya Ubunge, Hao ni:
* Dr Benjamin Mbeba.
* Mwl Bernard Merumba.
* Ndg Kennedy Chiguru.
* Advocate Zakayo Majinge.

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI LINAENDELEA KUHITAJI MAENDELEO YA JAMII YAKE YANAYOLETWA NA SERIKALI YA CCM. 

Tarehe 29.10.2025
USHINDI MKUBWA KWA CCM!

Imetolewa na:
Timu ya Kampeni
Jimbo la Musoma Vijijini 

Sun, 26 Oct 2025


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA