.Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi –INEC imewataka Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura nchini kufuata sheria, miongozo, taratibu na maelekezo ya Tume wakati wa utekelezaji wa majukumu ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025.
Maelekezo hayo kwa watendaji wa Uchaguzi nchini, yametolewa na Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Mahakama ya Rufaa MH. JACOBS MWAMBEGELE wakati alipotembelea, kukagua na kushuhudia mafunzo ynayofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya MPANDA mkoani KATAVI ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.
Akizungumza na watendaji hao wanaohudhuria mafunzo ya siku tatu ya Uchaguzi, JAJI MWAMBEGELE ametaja uadilifu na uaminifu kuwa ni miongoni mwa vigezo vilivowafnya kuteuliwa, hivyo watekeleze majukumu yao bila upendeleo.

Comments