Shamra Shamra, nderemo vikiwa vimetawala katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Kinyerezi, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Oktoba 22, 2025. Mkutano huo umeshirikisha wananchi wa majimbo manne ya Ilala, Ukonga, Segerea na Kivule.
Dkt. Samia katika kampeni zake amekuwa akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura bila woga Oktoba 29, 2025, akiwahakikishia usalama wa kutosha na kwamba atakayediriki kusababisha vurugu atakiona na moto, kwani vyombo vya ulinzi na usalama viko imara.
Comments