Shamra Shamra, nderemo vikiwa vimetawala kwenye Uwanja wa Leaders Club Kinondoni Dar es Salaam katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri y Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 21, 2025.
Dkt. Samia katika kampeni zake amekuwa akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura bila woga Oktoba 29, 2025, akiwahakikishia usalama wa kutosha na kwamba atakayediriki kusababisha vurugu atakiona na moto, kwani vyombo vya ulinzi na usalama viko imara.
Comments