NAJISIKIA RAHA KUONA BARABARA YA MWENDOKASI YA GONGO LA MBOTO - DKT. SAMIA



Mgombea Urais kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa huwa anajisikia raha anapoona barabara ya Mwendokasi ya Gongo la Mboto - Posta anapopita kutoka Uwanja wa Ndege kwenda Ikulu Dar es Salaam, lakini huchukizwa kuona makundi ya abiria wakisubiri daladala katika njia hiyo.


Dkt. Samia ameyasema hayo alipokuwa akijinadi yeye na wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho, katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Kinyerezi, Ilala jijini Dar es Salaam leo Oktoba 22, 2025.

Aidha, Dkt. Samia amewahakikishia usalama wananchi kwamba vyombo vya Ulinzi na Usalama ndani ya Taifa hili vimejipanga vyema na kwamba amevijengea uwezo wa kutosha, hivyo wasiwe na hofu watoke kwenda kupiga kura Jumatano Oktoba 29.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

RAIS SAMIA AMZAWADIA NYUMBA SIMBU