Kati ya vitu ambavyo vina pesa basi ni eneo la burudani hasa soka. Fikiria mishahara ya wachezaji kwasasa hapa Tanzania halafu kule Ulaya. Tanzania kwasasa kuna wachezaji wanalipwa pesa zaidi ya CEOs kibao nchini.
Baada ya kufanya mageuzi ya kiuongozi, ni rasmi sasa Billionea Patrice Motsepe ambaye ni Rais wa CAF amedhamiria kuvifanya vilabu vya Afrika vinavyoshiriki mashindano ya CAF kunufaika zaidi.
Kwasasa vilabu vyote vinavyoshiriki michuano ya CAF (Klabu Bingwa & Shirikisho) wa hatua za awali (Preliminary Stage) zinapata $ 50,000.
Pia kwa sasa kila klabu inayoshiriki hatua ya makundi kwenye shirikisho inapata $ 400,000.
Kwa timu za Azam FC na Singida Black Stars zitaleta nchini $ 800,000 sawa na TZS 1.96bn
Simba SC na Yanga SC zitapokea kila moja $ 700,000 ikiwa ni $ 1,400,000 sawa na TZS 3.43bn
Kwahiyo kwa ujumla vilabu vya Tanzania kwa kufikia hatua tu ya makundi kwenye michuano ya CAF vitaingiza jumla ya TZS 5.39bn tu!
Ikiwa vitafuzu kwenda Robo Fainali fedha hizo zitaongezeka mara dufu. Je, bado huioni pesa kwenye soka? Hiyo ndiyo maana mpira pesa!
Endapo tutawekeza zaidi kwenye michezo hasa soka, basi tutaweza kutatua tatizo la ajira kwa vijana nchini na kutengeneza uchumi imara.
Pesa nyingi kwenye burudani na michezo ambazo zinaelea!

Comments