ZAIDI YA WATU MIL.57 WAMEFUATILIA KAMPENI ZA CCM

ZAIDI ya Watu milioni 57 wamefuatilia kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi.

‎ Namba za kimtandao zinaonesha kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kampeni amefuatiliwa mara milioni 164.9. Hii inadhihirisha ukubwa wa CCM lakini kukubalika kwa mgombea huyo.

‎Hayo yamelezwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi alipokuwa akitoa tathmini na mrejeshi wa kampeni hizo kwenye ujumbi wa BOT jijini Mwanza leo Oktoba 27, 2025.

‎Pia, alisema mamilioni ya Watanzania walijumuika na CCM katika kampeni kwani Chama kinajivunia ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano kwani imekuwa rahisi idadi kubwa ya watu kufikiwa.

‎Aidha, Kihongosi amesema kuwa waliotufuatilia kupitia redio, televisheni, magazeti, mitandao na simu, kompyuta na vifaa vingine vya kidigitali ndani ya vyombo vya usafiri vibanda umiza.

‎"Mgombea wetu wameshafanya mikutano zaidi ya 114 ya kampeni yote imekuwa na mafanikio makubwa viwanjani. Msafara wa mgombea wetu Dk. Samia umeweza kusimamishwa maeneo mengi.

‎"Wananchi wakiwa na shauku ya kumuona mgombea, kumsikiliza na yeye hakusita kuweza kuzungumza na Watanzania pindi alipokuwa akisimamsishwa. Ameonesha utu wa kuwajali watu anaowahudumia na kuwaomba ridhaa."Amesema Kihongosi



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA