AFA BACHELA KWA KUCHAGUA MKE ALIYEKAMILIKA



MWANAUME ALIYECHAGUA SANA MKE


Aliulizwa mwanafalsafa mmoja:

“Unawezaje kumchagua mke?” 🤔


Akasema:


Sitaki awe mzuri kupita kiasi hadi wengine wamtamani, wala sitaki awe mbaya sana hadi nafsi yangu ikachukizwa naye.


Sitaki mrefu sana mpaka ninyanyue kichwa kumwangalia, wala mfupi sana hadi nainame kumtazama.


Sitaki mnene sana mpaka azuie upepo wa baridi, wala mwembamba sana hadi nimdhanie ni kivuli.😊


Sitaki mweupe kama mshumaa, wala mweusi kama kivuli cha usiku.


Sitaki mjinga kiasi kwamba ashindwe kunielewa, wala mwenye elimu kunishinda kiasi cha kunibishia kila mara.


Sitaki tajiri hadi aseme: “Hio ni mali yangu,” wala masikini kiasi cha kuwatesa watoto wangu baadaye.


Sitaki mkali mwenye hasira ngumu kuridhika, wala sitaki mwenye matakwa mengi asiyekoma kudai kila wakati.


Sitaki mkorofi anayepiga kelele nyumba ikatetemeka, wala sitaki mkimya kupita kiasi hadi asisikike kabisa.


👀 Inasemekana yule mwanafalsafa Mzee maskini alikufa bila kuoa. 🙄


MAFUNZO 👇


1.Hakuna mtu mkamilifu duniani


Kama mtu atatafuta mke (au mume) asiye na dosari hata kidogo, atamaliza maisha yake akimtafuta bila mafanikio. Binadamu wote tuna mapungufu, na ndoa inahitaji kukubali ukweli huo.


2.Ndoa haijengwi kwa vigezo vya mwili au mali pekee


Mwanafalsafa aliorodhesha sifa za mwili, tabia, mali, elimu… lakini ndoa ya kweli hujengwa zaidi kwenye maelewano, heshima, subira na upendo. Ukizingatia vigezo vya nje pekee, hutawahi kuchagua mtu.


3.Watu wanaotaka kila kitu kiwe “perfect” huishia kupoteza vyote


Ukiwa na masharti mengi kupita kiasi katika maisha iwe ndoa, kazi au urafiki unaweza kupitwa na fursa nzuri. Wakati mwingine, kukubali dosari ndogo ndogo ndio mwanzo wa kupata furaha.


Je wewe Bachela Mwenzangu ambaye bado unatafuta waubani wakumuweka ndani unapenda atakayekuja kuwa mke wako awe na sifa zipi?😄


Follow 👉 Sufian Mzimbiri  uweze kujifunza unayo yajua na usiyo yajua


#SufianMzimbiri

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

JESHI LA POLISI LATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA, LAONDOA KIZUIZI CHA KUTOTOKA NJE BAADA YA SAA 12 JIONI