Mafunzo hayo ya siku tano yanalenga kuwajengea uwezo Waheshimiwa Wabunge kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo Uendeshaji wa Shughuli za Bunge, Umuhimu wa Kamati za Bunge katika kufanikisha Shughuli za Bunge na Maadili ya Viongozi.
Masuala mengine ni kuhusu Haki na Wajibu wa Wabunge, Diplomasia na Itifaki za Kibunge pamoja na Mahusiano ya kazi baina ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Bunge.











Comments