UFAFANUZI DHIDI YA WANAOJARIBU KUFANYA UPOTOSHAJI KATIKA HOTUBA YA RAIS DKT. SAMIA NA MISINGI YA KUJENGA TAIFA LETU


Baraka Mussa, Kigoma Mjini

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa tarehe 14 Novemba 2025 wakati wa kufungua rasmi Bunge la 13 ni rejea muhimu sana  katika historia ya taifa letu. Ni hotuba iliyojaa dhamira ya kweli, upendo na misingi ya juu ya uongozi katika kulijenga Taifa letu. Kwa kiwango chochote cha uchambuzi, ni hotuba inayostahili kuhesabiwa katika kundi la *statecraft speeches* yaani hotuba za marais zinazojenga msingi wa taifa baada ya misukosuko.


Kwa bahati mbaya, baadhi ya wasomi, wanasiasa na viongozi wa dini wanajaribu kupotosha maana na umuhimu wa hotuba hii. Wamejikita katika hoja zisizo na msingi kisheria au kiutawala. Basi kama ilivyokawaida yetu tumeandika Makala ikilenga kuweka mambo sawa, na kusaidia jamii na vijana  kuelewa dhamira halisi ya hotuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.



*1. RAIS KUANZA HOTUBA YAKE KWA KUOMBOLEZA NI ISHARA YA UPENDO NA HURUMA*


Rais Samia alianza hotuba yake kwa kusimamisha Bunge zima dakika moja kuomboleza vifo vilivyotokea katika vurugu za tarehe 29 -30 Oktoba 2025. Kwa kufanya hivyo, Mama aliweka misingi ya kwanza ya uwajibikaji wa kihisia (moral responsibility) ambao ni sehemu muhimu ya uongozi wa kitaifa.


Mwanafalsafa maarufu na msomi mkubwa ambaye amekuwa professor katika vyuo kama Harvard, Brown, Chicago n.k  _Martha Nussbaum_ aliwahi kusema :- *“Nation-building begins with shared grief before shared ambition”* yaani, kujenga taifa huanza kwa kuungana katika maombolezo yanapotokea  kabla ya kuungana katika malengo yanayokuja.


Hii ni hatua inayotambulika duniani kote. Kwa mfano, baada ya vurugu za Capitol Hill nchini Marekani mwaka 2021, ambapo watu walifariki, Rais Biden alianza hotuba yake kwa msisitizo juu ya maombolezo. Kitendo cha Rais Dkt. Samia ni mfano wa uongozi wa kiutu na kiunganishi.



*2. KILICHOTOKEA TAREHE 29/30 OKTOBA NI VURUGU, SIO  MAANDAMANO*


Rais alisema *"Naomba tutumie dakika moja kuwaomboleza ndugu zetu waliopoteza maisha katika Vurugu zilizotokea siku ya Uchaguzi 29 au 30 Oktoba."*


Kwa umakini, Naungana mkono na mimi binafsi ninaamini kilichotokea sio maandamano ya amani ni vurugu au unaweza kuuta maandamano ya Vurugu. Kisheria, Maandamano ni mikusanyiko ya amani, isiyoharibu mali, isiyoleta hatari kwa watu na isiyovunja utulivu wa umma. Hii ndiyo maana ya *“peaceful assembly”* chini ya Katiba ya Tanzania, Ibara ya 20(1), na masharti ya *Police Force and auxiliary services Act*. Kinyume chake, tukio la 29/10/2025 lilihusisha kuchoma magari, vituo vya mafuta, viwanda, maduka na kuharibu huduma za umma. Huu ni *riot,* yaani vurugu, kama kifungu cha 74 cha Penal Code kinavyosema.


Hoja kwamba walikuwa wanandamana kwa amani ni hoja isiyo na msingi na sio sahihi .Na vyema wote tuseme kichotokea tarehe 29- 30 oktoba 2025 ni Vurugu na sio maandamano au tunaweza kuita vurugu za maandamano sio vyema au sahihi kuita maandamano hakuna maandamano ya namna ile Zile ni vurugu.


*3. SERIKALI KUUNDA TUME SIO KUJICHUNGUZA, NI KUCHUNGUZA UKWELI NA KUJENGA TAIFA LETU*


Kumekuwa na madai ya kupotosha kwamba *“serikali haiwezi kuunda tume kwa sababu itajichunguza yenyewe.”* Hili halina msingi. Kisheria na kiutawala, tume za uchunguzi huundwa na serikali kwa sababu serikali pekee ina mamlaka ya kikatiba ya kuunda tume, kuipa uwezo, na kuhakikisha inafanya kazi bila hofu au upendeleo. Tume haiwezi kujiunda yenyewe .


Tume ni chombo huru kinachoendesha uchunguzi wake, sio kundi la viongozi wa chama cha CCM au mawaziri. Ndiyo maana Rais Samia alisema itaundwa *“Enquiry Commission”*, tume rasmi, yenye wataalamu, yenye mamlaka ya kuuliza maswali na kutoa mapendekezo. Lengo la tume sio kutafuta mchawi, bali kujua ukweli wote: nini kilisababisha vurugu, nani alihusika na tufanye nini kama taifa ili jambo lisitoke tena.


Tume kama hizi zimeundwa katika nchi nyingi hata majirani zetu Kenya baada ya ghasia za uchaguzi, Afrika Kusini baada ya tukio la Marikana, Marekani baada ya shambulio la 9/11 na Uingereza katika matukio ya kiusalama. Popote pale, serikali ndiyo huunda tume lakini tume huchunguza kwa uhuru, bila kupendelea upande wowote. Kwa hiyo hoja kwamba serikali inajichunguza yenyewe ni propaganda tu, isiyo na msingi wowote.


*4. WITO KWA WATANZANIA NI KUUNGANA NA RAIS DKT. SAMIA  KATIKA KUJENGA TAIFA*


Kwa Watanzania wenzangu, tume hii ni daraja la taifa kuelekea ukweli, amani, na maridhiano. Rais Samia ametufundisha wazi kuwa taifa linajengwa kwa ukweli, mshikamano na ushirikishwaji, sio kwa mapigano, uharibifu, au vurugu. Kila mmoja anapaswa kuelewa, kuthamini na kuunga mkono jitihada hizi, akiachana upotoshaji na uongo unaoenezwa mitandaoni pia, tuungane na Rais Dkt.Samia.


Ukweli ni kwamba, Hotuba ya Rais Samia imejaa busara, upendo na dhamira ya kuijenga Taifa letu. Migogoro inaweza kutokea, lakini amani lazima ilindwe tuu. Kuna wanaojaribu kupotosha, lakini ukweli lazima ushinde tuu. Tanzania ni yetu sote na Mama ameonyesha njia sahihi ya maelewano, msamaha, utu na umoja wa kitaifa. *Tuungane naye*


*

*Mungu Ibariki Tanzania,  Mungu dumisha Haki, upendo amani na maelewano katika taifa letu, Aamiin*


Itaendelea...

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

JESHI LA POLISI LATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA, LAONDOA KIZUIZI CHA KUTOTOKA NJE BAADA YA SAA 12 JIONI