Walokole wengi wanaishi maisha magumu kwa sababu baada ya kuokoka;
1.Walokole wengi baada ya kuokoka wamekosa nafasi ya kufanyiwa maombi ya deliverance. Walokole wengi sana wapo kwenye vifungo kwenye nafsi zao walivyovipata kabla ya kuokoka kutokana na madhabahu za koo zao, uchawi, uganga ,ushirikina waliofanyiwa huko nyuma.
Vifungo vya kwenye nafasi haviondoka kwa kuokoka pekee, baada ya kuokoka inabidi ufuate mchakato wa ukombozi. Ukombozi maana yake kurejesha vilivyoibiwa, vilivyoharibiwa au vilivyouwawa na adui ( Yohana 10:10)
Mtu anapookoka roho yake ndiyo inayookoka, baada ya kuokoka nafsi yake ndiyo inayotakiwa kushughulikiwa kutoka kwenye vifungo vya ukoo, uchawi, uganga, ushirikina n.k. Walokole wengi sana wanaishi maisha ya vifungo wakidhani ni mapito. Kuna tofauti kati ya mapito na vifungo.
Hata kama umeokoka usipotolewa kwenye misingi ya ukoo wenu ambao ulikushikilia hata kabla ya kuokoka kwako utaishi maisha yaleyale wanayoishi ndugu zako ambao hawajaokoka kutokana na vifungo vya ukoo wenu kama vile Kuna wengi kwao vifungo vyao ni umasikini, vifo vya mapema, magonjwa fulani, kuishia kiwango fulani cha elimu, kutooa/ kutolewa n.k
Kuokoka ni jambo moja, kuondolewa kwenye vifungo ni jambo lingine kabisa. Usipoondolewa kwenye vifungo, mtumishi wa Mungu Mwl. Christopher Mwakasege huwa anapendelea kusema mbinguni utaenda ila kwa kuchoka sana.
N.B Pointi hii wenye ufahamu mkubwa wa kiroho ndio watakaoielewa ila wenye ulokole wa mapokeo ni ngumu kuielewa maana wanasimamia kuwa ukiokoka yote yamekwisha na kusahau kuwaombea watu maombi ya ukombozi baada ya kuokoka.
Siku moja 2026 nitafundisha kwa ukubwa kuhusiana na umuhimu wa huduma/ maombi ya ukombozi baada ya kuokoka ili shetani asiendelee kuyatesa maisha yako.
2.Kukosa uhusiano binafsi na Mungu kupitia Bwana Yesu na Roho Mtakatifu mwenye hatima zao za maisha AU kuwa na ulokole wa mazoea.
Waebrania 2:3
Yohana 15:7
3.Kutomjua Mungu kibinafsi ( kumjua Mungu na neno lake).
Ayubu 22:21
4.Kutomsikiliza na kumtii Mungu Mungu
Isaya 1:19
Watu wote kwenye biblia waliofanikiwa ni kwa sababu walimsikia Mungu na kutii maelekezo yake/ sauti yake. Mfano Ibrahimu alitii sauti ya Mungu iliyomwambia aondoke kwao aende mpaka kwenye nchi atakayomwonyesha.
5.Kutoongozwa na Roho wa Mungu.
Ukishaokoka kufanikiwa kwako hapa duniani ni kwa kuongozwa na Roho wa Mungu maana Roho wa Mungu ndiye anayejua kila kitu ulichopangiwa hapa duniani.
1 Wakorintho 2:10-12
Warumi 8:14
6.Kukosa maarifa/ kutojua maandiko.
Kukosa maarifa ya kiMungu kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao kama vile biashara, utumishi, huduma n.k Maarifa ya neno la Mungu ndio ufunguo mkubwa wa kufanikiwa kuishi kwenye maisha ambayo Mungu ametupangia.
Walokole wengi ni wavivu wa kusoma neno la Mungu, vitabu mbalimbali vya neno la Mungu n.k
Hosea 4:6
Mathayo 22:29
7.Kutoishi kwa kuzingatia kanuni za kiMungu AU kutoishi maisha ya kujidhabihu ipasavyo mbele za Mungu kama vile kufunga na kuomba,kujaa neno la Mungu, utakatifu, utoaji wa sadaka, maisha ya ibada n.k
8. Kuishi nje ya hatima zao za maisha walizopangiwa na Mungu/ kuishi nje ya kazi zao walizoumbiwa na Mungu mfano kama umeumbwa kuwa mfanyabiashara lakini ukaenda kuwa mwajiriwa kwenye hiyo ajira utakosa neema na Mungu hatakuwa pamoja na wewe kwa kuwa umeenda sehemu ambayo hajakuita.
Kuishi nje ya hatima ya maisha uliyopangiwa na Mungu/ nje ya kusudi la kuumbwa kwako ni lazima utapata mahangaiko sana maishani mwako kwa sababu unakuwa unaishia nje ya neema uliyokusudiwa. Walokole wengi hawajui kusudi la kuumbwa kwao.
Mfano mzuri tunauona kwa Yona alivyopatwa na misukosuko mingi sana alipotaka kukimbia wito au hatima yake ya maisha aliyekuwa amepangiwa na Mungu.
Hata leo hii walokole wengi wana misuko suko mingi kwenye maisha yao kwa sababu ya kuishi nje ya wito wao walioitiwa hapa duniani.
9. Walokole wengi hawajui kuomba/ hawaombi sawasawa na mapenzi ya Mungu ndio maana hawapokei kutoka kwa Mungu. Kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu ni kuomba kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu na kuomba sawasawa na neno lake.
Warumi 8:26-28
Yakobo 4:3
10. Walokole wengi hawana nguvu za kuuteka ufalme wa Mungu ndani yako ambao utawasaidia kupenya kirahisi kwenye mambo yao hapa duniani. Na ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu za kiroho. Ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu ndani ya mtu kupitia Roho wa Mungu.
11. Walokole wengi hawawaheshimu watumishi wa Mungu/ hawajui umuhimu wa nafasi za watumishi wa Mungu kama wapagani wanavyothamini nafasi za waganga wao kwao.
2 Mambo ya Nyakati 20:20
Baraka za maisha yetu kutoka kwa Mungu zinaachiliwa kupitia vinywa vya watumishi wa Mungu, neema mbalimbali tunazozihitaji maishani mwetu zipo kwa watumishi wa Mungu waliopakwa mafuta.
Tunaona Daudi alifanikiwa kuwa mfalme kwa sababu ya nafasi ya mtumishi wa Mungu nabii Samweli kwenye maisha yake.
Hii iwe kanuni ya maisha yako usianze jambo lolote lile kama vile huduma, biashara, nafasi ya uongozi, kufanya interview bila kwenda kwa mtumishi wa Mungu.
Wana wa giza wanafanikiwa sana kwa sababu wanawaheshimu na kutii maelekezo ya makuhani wao wakiwemo waganga.
12. Kutokua kiroho kwa ujumla nako kunawafanya walokole wengi kuishi maisha ya kutofanikiwa. Kadri unavyoongezeka kiroho ndivyo kadri unavyokuwa na mamlaka na sauti katika ulimwengu wa roho zitakazokusaidia kushishinda vita za kiroho zinazokuzuia kuishi maisha uliyopangiwa na Mungu.
Waefeso 6:12
13. Kutoishi maisha ya kuenenda katika Roho. Maisha ya kutimiza tamaa za mwili ni kikwazo sana kwa walokole wengi kuishi maisha waliyokusudiwa na Mungu. Matendo ya mwili yanakuwa ni mizigo mizito inayowazuia walokole wengi kupaa kwenye kiwango cha maisha walichokusudiwa na Mungu hapa duniani.
Kuna tabia za kimwili ambazo zimetajwa ambazo zimetajwa kwenye kitabu cha Wagalatia 5:16-25 ambazo zinapunguza utendaji nguvu za Mungu kufanya kazi ipasavyo maishani mwa walokole wengi ambazo zingewafanikisha kwa ukubwa maishani mwao.
Maisha ya makando kando ni kuzuizi pia cha kufanikiwa kwa walokole wengi.
14. Kutoishi maisha ya kujaa Roho Mtakatifu, upako wake na nguvu zake. Ni vigumu sana kwa mlokole kufanikiwa hapa duniani bila Roho Mtakatifu, upako wake na nguvu zake. Mfano mzuri tunauona kwa Bwana Yesu alianza kufanya maajabu/ kuwa na MAFANIKIO baada ya maisha yake kuvuviwa na Roho Mtakatifu, upako wake na nguvu za zake.
15. N.k
NI MAPENZI YA MUNGU KUONA WATOTO WAKE WALIOKOKA KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO KILA ENEO LA MAISHA YAO.
3 Yohana 1:2
Ila kumbuka kuwa ndani ya safari ya wokovu kuna kipindi cha mapito ambacho huwa kina mwisho wake. Pia usipokuwa na ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu unaweza ukawa kwenye kifungo ambacho kinadumu maisha yako yote ukadhani ni mapito.
POINTI HIZI ZOTE NI NGUMU KUELEWEKA KWA WALOKOLE WA KIMAPOKEO/ AU WANAOKARIRI MAANDIKO KULIKO KULIJUA NENO.
ACHA UJUAJI KWENYE NENO LA MUNGU. PIA USIKOMENTI KIMHEMKO KWENYE FUNDISHO LINALOTOKANA NA MAFUNUO YA ROHO MTAKATIFU NA UVUVIO WAKE MAANA ATAKUFUNDISHA VITU AMBAVYO VINATOFAUTIANA NA ULIVYOKALILISHWA KANISANI KWAKO KUTOKANA NA MAPOKEO.

Comments