WENYEJI, Morocco wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mali katika mchezo wa Kundi A Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku huu Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.
Winga wa Real Madrid ya Hispania, Brahim Abdelkader Dรญaz alianza kuwafungia Simba wa Atlasi dakika ya akimtungua kwa mkwaju wa penalti kipa wa Yanga SC ya Tanzania, Djigui Diarra.
Lakini mshambuliaji wa AJ Auxerre ya Ufaransa, Lassine Sinayoko akawasawazishia Tai dakika ya kwa penalti pia akimchambua kipa mzaliwa wa Canada, Yassine Bounou wa club Al Hilal ya Saudi Arabia.
Kwa matokeo hayo, Morocco inafikisha pointi nne kufuatia ushindi wa 2-0 dhid ya Comoro kwenye mchezo wa kwanza, wakati Mali inafikisha pointi mbili kufuatia sare nyingine ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza na Zambia.
FULL-TIME! ๐ฒ๐ฆ๐ฒ๐ฑ Morocco 1-1 Mal๐ค
#TotalEnergiesAFCON2025 |

Comments