Haijalishi mkeo anafanya kazi na anapata pesa au hafanyi kazi, jukumu kumtunza yeye na familia yako ni lako wewe mwanaume.
Mwanaume anatakiwa kuogopa umasikini ambao utamfanya adharirike na familia yake kuishi kwa shida.
Kama mwanamke hakuheshimu kamwe hakufai na hatakufaa popote pale.
Katika maisha yako usije kumtelekeza mtoto, iwe umempata kwa bahati mbaya au maisha yako magumu tunza mwanao, usije ukamkimbia.
Hakikisha una vyanzo zaidi ya kimoja vya kukuingizia pesa, dunia haina huruma kwa mwanaume Maskini.
Kama wazazi wako wapo hai hakikisha hata mara moja moja unawatumia pesa, sio lazima wakuombe, kuwa na utaratibu tu wa kuwatumia pesa hata pale wasipokuomba. Labda kama wazazi wako ni matajiri na hawana shida na pesa yako.
Kama upo na binti na unajua humuoi, usimrubuni kwa kumwambia utamuoa.
Hata kama upo busy vipi, hakikisha unapata muda wa kufurahia na familia yako.
Siku moja moja pata muda wa kufanya shughuri ndogo ndogo za nyumbani, msaidie mkeo kazi za nyumbani mbele ya watoto wako hasa wa kiume, hapa utakuwa unatengeneza wanaume bora kwa wake zao huko mbele.
Usiendekeze pombe, utaharibu maisha yako.
Kuwa na msimamo hasa katika kutekeleza malengo yako.
Usivumulie kuvunjiwa heshima popote pale.
Shiriki shughuli za kijamii katika jamii yako, sherehe, misiba na mambo mengine.
Linda familia yako kwa gharama yoyote ile.
Familia yako iwe kipaumbele namba moja katika maisha yako.

Comments