WADAIWA KODI YA ARDHI KIKAAONGONI

*Waziri Akwilapo Ataka Kukamilisha malipo ifikapo Desemba 31, 2025

*Aagiza Vituo vya Makusanyo ya Kodi kutoa huduma bora

MASASI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo ameelekeza wadaiwa wote wa Kodi ya Pango la Ardhi nchini wawe wamekamilisha malipo ya madeni yao kufikia  Desemba 31, 2025.

Akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Masasi mkoani Mtwara leo tarehe 23 Desemba 2025 Mhe. Dkt Akwilapo amesema, kuchelewa kulipwa kodi ya pango la ardhi kutasababisha wamiliki wa ardhi kuwa na malimbikizo ya madeni pamoja na riba. 

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, madhara mengine yanayoweza kutokea kwa wamiliki ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kufutiwa umiliki wa ardhi. Hatua hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya ardhi Sura ya 113 Fungu la 48 (1), 50,  51 na 52.

Mhe. Dkt Akwilapo ameelekeza vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi katika ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri nchini kuhakikisha vinatoa huduma bora za kuwasaidia wananchi wanaopata changamoto za kulipa kodi hiyo kwa kuzingatia utu pale wanapotekeleza majukumu yao.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

NAMNA YA KUTENGENEZA MAISHA YAKO KIMYA KIMYA

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

Wasifu wa Kizza Besigye

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA

HAKUNA DHEHEBU LA DINI AMBALO LIKO JUU YA LINGINE, MADHEHEBU YOTE YAKO SAWA KISHERIA - RAIS SAMIA