ASHINDA UBUNGE AKIWA GEREZANI UGANDA


Msemaji wa Chama Cha National Unity Platform (NUP) ,chama Kikuu cha upinzani Uganda, Alex Waiswa Mufumbiro ameshinda nafasi ya Ubunge wa jimbo la Nakawa Mashariki katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jana Jan 15 nchini Uganda. 

Msemaji huyo mwaka jana 2025 alikamatwa akiwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kawempe, Kampala alipokwenda kuhudhuria kesi ya Eddie Mutwe, ambae ni mkuu wa na ulinzi wa Bobi Wine, ambapo Alex Waiswa Mufumbiro akaunganishwa katika kesi na Eddie Mutwe, wakatunzwa gereza la Luzira, Kampala na hawajawahi kuachiwa huru Mpaka sasa. 

Akiwa ameishi gerezani kwa siku 78 hadi sasa, bado wananchi wa Nakawa Mashariki, Kampala, wamemchagua Ndug.Alex Waiswa kuwa mbunge wao kupitia chama National Unity Platform (NUP) akiwa bado gerezani.

#rockdigitalupdates #habari #uganda #election


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

IJUE HISTORIA YA MCHEZAJI MZUNGU WA TANZANIA