BENKI YA NMB YAZINDUA AGENDA 2030,YAVUNA FAIDA YA SH.TRILIONI 1.1 MKAKATI ULIOPITA (MTP 2025)

 BENKI ya NMB imezindua Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Mwaka 2026 hadi 2030 (Agenda 2030), huku ikitangaza mafanikio yaliyotukuka ya Mpango Mkakati uliopita (MTP 2025), iliyoufunga kwa faida ya kihistoria ya Mapato Kabla ya Kodi (PBT) ya Sh. Trilioni 1.13 kwa mwaka wa Fedha ulioishia Desemba 31, 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Agenda 2030, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema wanajivunia mafanikio makubwa ya jumla katika kipindi cha miaka mitano, waliofunga kwa kuvuna faida ya Sh. Trilioni 1.1 ambayo nis awa na ongezeko la asilimia 15.

Katika mchanganuo wake, Bi. Zaipuna alifafanua kuwa Faida Baada ya Kodi kwa mwaka 2025 ni Sh. Bilioni 750 ambalo ni ongezeko la asilimia 16, huku Mapato Yote ya Taasisi hiyo yakiwa ni Sh. Trilioni 1.82 (ongezeko la asilimia 11) na Mali zote za benki zikiwa na thamani ya Sh. Trilioni 17.2.

“Kwa kipindi chote cha utekelezaji wa MTP 2025, NMB imepata matokeo madhubuti, yaliyojumuisha utendaji imara wa kifedha na mchango mpana katika kuchochea na kuwezesha shughuli za kiuchumi,” alisisitiza Bi Zaipuna na kufafanua kuwa:

“Katika kipindi hicho cha miaka mitano, benki ilizalisha faida ya jumla ya Sh. Trilioni 2.7, huku mikopo yote iliyotolewa ilikuwa na thamani ya zaidi ya Sh. Trilioni 27.6, Amana za wateja zilifikia kiasi cha Sh. Trilioni 12.4, huku akaunti za wateja zikiongezeka hadi kufikia Mil. 9.9,” alisema.

Bi. Zaipuna alisema benki yake inajivunia mafanikio iliyopata katika MTP 2025, na kwamba ana imani kubwa kwamba MTP 2030 utakuwa kichocheo cha ukuaji bora wa NMB, akiamini unaenda kujenga benki imara yenye ukuaji endelevu wenye kuakisi mahitaji ya soko ya sasa na baadae.

“Mpango Mkakati huu mpya umejengwa juu ya mafanikio yaliyopatikana, na unaweka dira ya ukuaji endelevu unaoongozwa na Mteja, Teknolojia, na Tija ya Kiutendaji. Katika kipindi hiki kipya cha kimkakati, tutaweka mkazo mahususi katika maeneo yafuatayo;

“Kuboresha kwa kiwango cha juu huduma kwa wateja, kuimarisha mabadiliko ya kidijitali na matumizi ya kimkakati ya Data, kufadhili Sekta za Kimkakati zinazochochea Ajira, Uzalishaji, na ongezeko la thamani katika Uchumi, ikiwemo Sekta ya kilimo, Ujenzi, Vwanda, Utalii na Sekta za Nishati na Madini.

“Lakini pia mpango huu unaenda kupanua wigo wa shughuli zetu nje ya huduma za sasa za kibenki, pamoja na kupanua wigo wa benki yetu nje ya mipaka ya Tanzania. Sasa tunakwenda kuwekeza na kuipeperusha bendera ya Tanzania katika viwango vya ubora na ufanisi nje ya Tanzania,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Msajili wa Mgeni Rasmi wa hafla ya uzinduzi huo, ambaye ni Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wa NMB kwa mafanikio yaliyotukuka ya MTP 2025, sambamba na yale ya mwaka hadi hadi.

Mchechu aliitaja kama kiongozi sahihi wa Sekta ya Fedha katika kuyaendea na kuyafanyia kazi maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye alimtuma kufikisha salamu za pongezi kwao kutokana na ufanisi na mafanikio makubwa waliyopata.

“Hili nilitakiwa nilianze kulisema kabla ya yotem kwa sababu niliaga kwa viongozi wangu. Mheshimiwa Rais anawasubiri kwa hamu kwenye gawio lake Juni mwaka huu. Kwa mafanikio haya, nina uhakika anatamani sana kukutana nanyi.

“Mimi nilitumwa niwapongeze, na hapa niseme tu kwamba Rais Samia anawapongeza na kuwashukuru sana sio tu kwa mafanikio makubwa mliyopata, bali kwa kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa uchumi endelevu wa nchi yetu.

“Tumeambiwa hapa kuwa gawio la Serikali kutoka NMB katika kipindi cha miaka mitano ya MTP 2025 ni Sh. Bilioni 224, niseme tu mbele yenmu kwamba sio hizo pekee, NMB imetuzalishia Serikali kwa uwekezaji wetu kiasi cha Sh. Bil. 670 katika kipindi hicho cha miaka mitano.

Aliongeza ya kwamba Serikali inaitazama NMB kwa jicho la karibu sana, huku akiahidi kuwa watasimama imara katika kuhakikisha benki hiyo inakuwa na Bodi ya Wakurugenzi iliyo imara ili kuendeleza mafanikio hayo ya sasa kwa miaka kadhaa ijayo.

“Benki hii inaposema ina wawezekezaji wa kimkakati, ina maana tuko wawili wenye asilimia zaidi ya 30, kwa hiyo jicho letu Serikali tunaliweka kwa ukaribu sana NMB,” alisema Mchechu na kuongeza:

“Tutahakikisgha NMB ina Bodi Imara, tutaleta Wajumbe wa Bodi Mahiri, na ‘tunai-protect’ Bodi kutoka kwenye siasa zozote ambazo haziendani na biashara.

“Kama Mwanahisa wa NMB aliyeshika hisa za Serikali, nayazungumza haya kwa kina na ndio maagizo niliyonayo. Fanyeni kazi, leteni uzalishaji wenye tija, onesheni mfano kwa wengine na tutasimama nanyi katika kila hali, ingawa tunapenda mtuongoze kwenye raha,” alisisitiza Mchechu.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Benson Mahenya (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa kuanzia mwaka 2026 hadi 2030 uliopewa jina la Agenda 2030 wa Benki ya NMB. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Prof. Sylvia Temu na kulia ni Afisa Mkuu wa Fedha NMB, Juma Kimori. (Na Mpiga Picha Wetu).

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾