JWTZ YA TOA MSAADA NA HUDUMA YA AFYA KWA WANANCHI MSATA

.Mkuu wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Brigedia Sijaona muyala amewaongoza Ma afsa na Aksari wa Jeshi kutoa msaada kwenye jamii ya kitongoji Cha lukenge kilichopo Kijiji Cha kihangaiko kata ya Msata wilaya ya Bagamoyo Mkoa Pwani .

Msaada huo umetolewa kwa wananchi ikiwa ni zoezi la medani lijulikanalo kama EXERCISE MALIZA
Linalofanya na kuruti lenye lengo la kuimalisha mahusiano na wananchi wa eneo hilo.

Mkuu wa shule hiyo ya awali ya mafunzo ya kijeshi Brigedia muyala amesema zoezi Hilo la utoaji msaada kwa Jamii ni kuimalisha ushirikiano baina ya Jeshi na wananchi ikiwa pamoja na ulinzi na usalama kwa wananchi.

Brigedia muyala amesisitiza kuwa Jwtz kitaendelea kutoa misaada ya kibinadamu  pindi inapohitajika katika eneo lao ili kudumisha umoja na ushirikiano mzuri ulipo katika eneo kwa JWTZ na wananchi .

Aidha mganga wa hospital ya shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS kihangaiko meja Edwin Mboya amesema timu ya madaftari na wahudumu ilitoa elimu  na tiba kwa wananchi 200 sambamba kupatiwa matibabu pamoja na uchunguzi  wa afya na tiba.

Mwenyekiti wa kitongoji Cha kihangaiko Shabani Mkomo alipongeza JWTZ kwa msaada walioutoa kwa wananchi ambao umekuwa na manufaa makubwa lakini pia wanashukuru kwa kuendelea kudumisha uhusiano ulipo baina ya wananchi na Jeshi Hilo.

Baadhi ya wananchi nao kibwana mtiko na stela losai wameshukuru msaada waliopatiwa.

Jeshi la wananchi wa Tanzania limeendelea kutoa misaada mbalimbali pamoja na huduma kwa Jamii ikiwa lengo ni kudumisha uhusiano  na ushirikiano Tangu  kuhasisi tarehe 1 September 1964.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAPACHA WATATU FAMILIA YA MWAIKENDA WAPATA KIPAIMARA

MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 20

AINA 4 ZA WANAWAKE WASIOWEZA KUDUMISHA NDOA.

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

IJUE HISTORIA YA MCHEZAJI MZUNGU WA TANZANIA